Appendix C. Leseni ya Nyaraka Huru ya GNU

Table of Contents

0. UTANGULIZI
1. UTUMIKAJI NA FASILI
2. KUNAKILI BILA KUBADILISHA KITU
3. KUNAKILI KATIKA IDADI
4. MABADILIKO
5. KUJUMUISHA NYARAKA
6. MKUSANYIKO WA NYARAKA
7. KUJUMUISHA NA KAZI BINAFSI
8. TAFSIRI
9. USITISHAJI
10. MAREKEBISHO YA BAADAYE YA HII LESENI
Jinsi ya kutumia hii Leseni kwa ajili ya nyaraka zako

Toleo 1.1, Machi 2000

Copyright (C) 2000 Free Software Foundation, Inc. 51 Franklin St, Fifth Floor, Boston, MA 02110-1301 USA Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

UTANGULIZI

Lengo la hii Leseni ni kutengeneza mwongozo, daftari, au nyaraka nyingine iliyoandikwa "huru" katika hali ya uhuru: kumhakikishia kila mtu uhuru wa kunakili na kuisambaza upya, bila au kwa kuibadilisha, kwa biashara au sio kwa biashara. Kwa hali ya juu zaidi, hii Leseni inahifadhi kwa ajili ya mwandishi na mchapishaji jinsi ya kupata sifa kwa kazi zao, na sio kuonekana wahusika wa kubadili kaziza wengine.

Hii Leseni ni aina ya "nakilikushoto", ambayo inamaanisha kwamba kazi zitokanazo na nyaraka lazima nazo ziwe huru katika hali hiyo hiyo. Inaongezea kwenye GNU Genera Public Licence, ambayo ni leseni ya nakalakushoto iliyoundwa kwa ajili ya programu za bure.

Tumeunda hii leseni ili kuweza kuitumia kwa ajili ya miongozo ya programu za bure, kwa sababau programu za bure zinahitaji nyaraka za bure: programu ya bure lazima ije na miongozo inayotoa uhuru sawa na ule unaotolewa na programu. Lakini hii leseni haina kikomo kwa miongozo ya programu; inaweza kutumika kwa ajili ya kazi zozote za nakala, bila kujali mada au kwamba inachapishwa kama kitabu. Tunashauri hii leseni kwa kazi ambazo lengo lake ni maelekezo au marejeo.