UTUMIKAJI NA FASILI

Leseni inafanya kazi kwa mwongozo wowote au kazi nyingine ambayo ina notisi iliyowekwa na mmiliki wa hakimiliki inayosema inaweza kusambazwa chini ya makubaiano ya Leseni hii. "Waraka", hapa chini, unaashiria mwongozo wowote au kazi. Mwanachama yoyote wa umma ni mmiliki wa leseni, na anaitwa "wewe".

"Toleo Lililobadilishwa" la Nyaraka inamaanisha kazi yoyote yenye Nyaraka au sehemu yake, aidha nakala isiyobadilishwa, au yenye mabadiliko na/au iliyotafsiriwa kwenda lugha nyingine.

"Kifungu cha Sekondari" ni kiambatanisho kilichopewa jina au kifungu cha mambo ya mbele ya nyaraka, inayohusika kipekee na uhusiano wa mchapishaji au mwandishi wa nyaraka na kichwa cha habari cha ujumla cha nyaraka (au kwa mambo yanayohusiana), na haina kitu ambacho kinaweza kuingia moja kwa moja ndani ya kichwa cha habari cha ujumla. (Kwa Mfano, kama Nyaraka ni sehemu ya kitabu cha hisabati, Kifungu cha Sekondari hakiwezi kuelezea hesabu yoyote.) Uhusiano huo unaweza kuwa wa muunganiko wa kihistoria au mambo yanayohusika, au sheria, biashara, falsafa, maadili au nafasi ya siasa inayohusiana nazo.

"Vifungu Visivyoathirika" ni Vifungu fulani vya Sekondari ambavyo vichwa vyao vimeteuliwa, kama vile vya Vifungu Visivyoathirika, katika notisi isemayo nyaraka imetolewa chini ya Leseni hii.

"Nakala za Jalada" ni vifungu vifupi vya maneno ambavyo vimeorodheshwa, kama Nakala za Mbele za Jalada au Nakala za Nyuma za Jalada, katika notisi inayosema Nyaraka imetolewa chini ya Leseni hii.

Naka "Angavu" ya Nyaraka inamaanisha nakala inayoweza kusomwa na mashine, inayowakilishwa katika umbo ambalo ubainishwaji wake unapatikana kwa umma kwa ujumla, ambao maudhui yake yanaweweza kuonekana na kuhaririwa moja kwa moja na kwa urahisi kwa kutumia vihariri vya nakala za ujumla au (kwa ajili ya taswira zilizojengwa na pikseli) programu za uchoraji za ujumla au (kwa ajili ya michoro) baadhi ya vihariri vya michoro vinavyopatikana kirahisi, na ambavyo vinafaa kwa ajili ya ingizo la nakala kwenye vinavyoandaa umbizo au kwa ajili ya tafsiri otomatiki kwa maumbo mbali mbali, vinavyofaa kwa ajili ya ingizo la viandaa umbizo la nakala. Nakala iliyotengenezwa katika faili lenye umbizo Angavu, ambalo dhulisho mabadiliko yake imeundwa kuzuia au kukatisha tamaa maboresho ya wasomaji sio Angavu. Nakala ambayo siyo "Angavu" inaitwa "Isiyo angavu".

Mifano ya maumbo yanayofaa kwa ajili ya nakala Angavu inajumuisha: ASCII wazi bila dhulisho mabadiliko, umbizo la maingizo la Texinfo, umbizo la maingizo la LaTeX, SGML au XML kwa kutumia DTD inayopatikana kwa umma, na HTML ya kawaida iliyoundwa kwa ajili ya mabadiliko ya mwanadamu. Maumbo yasiyo angavu yanajumuisha: PostScript, PDF, maumbo binafsi ambayo yanaweza kusomwa na kuhaririwa na vichakatishi vya maneno binafsi tu, SGML au XML ambazo DTD na/au vifaa vya uchakatishaji havipatikani kwa ujumla, na HTML zinazozalishwa na mashine zinazotengenezwa na baadhi ya vichakatishi maneno kwa ajili ya matokeo tu.

"Ukurasa wa mbele" inamaanisha, kwa kitabu kilichochapishwa, ukurasa wa mbele wenyewe, kujumuisha na kurasa zinazofwata kama zinavyohitajika kushikilia, kusomwa, vitu ambavyo hii Leseni inahitaji vionekane kwenye ukurasa wa mbele. Kwa kazi zenye maumbo ambayo hayana ukurasa wa mbele wowote kama huu, "Ukurasa wa Mbele" inamaanisha nakala karibu ya muonekano muhimu wa kichwa cha habari cha kazi, kabla ya mwanzo wa kiini cha nakala.