KUNAKILI KATIKA IDADI

Kama ukichapisha nakala za Nyaraka zenye idadi zaidi ya 100, na notisi ya leseni ya nyaraka inahitaji Nakala za Jalada, unatakiwa kujumuisha nakala zinazobeba, zinazosomeka na kuonekana kwa urahisi, Nakala za jalada zote hizi: Nakala za Jalada la Mbele katika jalada la mbele, na Nakala za Jalada la nyuma kwenye jalada la nyuma. Majalada yote lazima yaonyeshe kiurahisi na kwa kusomeka kwamba wewe ndiyo mchapishaji wa hizi nakala. Jalada la mbele lazima lionyeshe kichwa cha habari kizima chenye maneno yote yenye usawa na kuonekana. Unaweza kuongeza vitu vingine kwenye jalada kwa nyongeza. Kunakili na mabadiliko yenye kikomo kwa jalada, ikiwa tu zinahifadhi kichwa cha habari cha nyaraka na kuridhisha masharti haya, inaweza kuchukuliwa kama kunakili bila mabadilko kwa upande mwingine.

Kama nakala zinazotakiwa kwa ajili ya majalada yote ni nyingi sana ili kutosha vizuri, unatakiwa kuweka za kwanza zikiwa zimeorodheshwa (nyingi kadri zitakavyotosha) katika jalada halisi, na kuendelea na zinazofwata katika kurasa za karibu.

Kama ukichapisha au kusambaza nakala Zisizo Angavu za Nyaraka idadi zaidi ya 100, lazima aidha ujumuishe nakala Angavu isomwayo na mashine pamoja na nakala Isiyo Angavu, au tamka kwenye au kwa kila nakala Isiyo Angavu eneo linalofikika na umma la mtandao wa kompyuta, lenye nakala kamili Angavu ya Nyaraka, isiyokuwa na nyongeza yoyote, ambayo mtandao wa ujumla wa umma una uwezo wa kupakua bila kujulikana, bila gharama yoyote, kwa kutumia kanuni za kawaida za mtandao wa umma. Kama ukitumia chaguo la mwisho, lazima uchukue hatua kwa uangalifu, ukianza usambazaji wa nakala Zisizo Angavu kwa idadi, kuhakikisha hii nakala Angavu itabakia ikipatikana katika eneo tajwa, mpaka angalau mwaka mmoja tangu mara ya mwisho umegawa nakala Isiyo Angavu (mwenyewe au kupitia mawakala wako au wauzaji wa rejareja) wa toleo hilo kwa umma.

Inaombwa na sio lazima, kwamba uwasiliane na waandishi wa nyaraka kabla ya kusambaza upya idadi kubwa ya nakala, kuwapa nafsi ya kukupa toleo lililosasishwa la nyaraka.