MABADILIKO

Unaweza kunakili na kusambaza Toleo Lililobadilishwa la Nyaraka chini ya masharti ya kifungu 2 na 3 juu, ikiwa kwamba unatoa Toleo Lililobadilishwa chini ya Leseni hii, na Toleo Lililobadilishwa likichukua jukumu la Nyaraka, hivyo usambazaji wa leseni na ubadilishaji wa Toleo Lililobadilishwa kwa yoyote anaemiliki nakala yake. Kwa zaidi, unatakiwa kufanya haya mambo kwenye Toleo Lililobadilishwa.

  1. Tumia katika Ukurasa wa Mada (na kwenye majalada kama yapo) mada tofauti kutoka ile ya Nyaraka, na zile za matoleo ya nyuma (ambazo zinatakiwa, kama zilikwepo kuorodheshwa katika kifungu cha Historia cha Nyaraka). Unaweza kutumia mada sawa na ya toleo la nyuma kama mchapishaji halisi wa toleo hilo akitoa ruhusa.

  2. Orodha kwenye Ukurasa wa Mbele, kama waandishi, mtu mmoja au zaidi au vyombo vilivyohusika na uandishi wa mabadiliko katika Matoleo Mapya, pamoja na japo waandishi wakuu watano wa Nyaraka (waandishi wakuu wote, kama ina chini ya watano).

  3. Tamka katika ukurasa wa mbele jina la mchapishaji wa Toleo Lililobadilishwa, kama mchapishaji.

  4. Hifadhi notisi za hakimiliki zote za Nyaraka.

  5. Ongeza notisi sahihi ya hakimiliki kwa mabadiliko yake karibu na na notisi nyingine za hakimiliki.

  6. Jumuisha, baada tu ya notisi za hakimiliki, notisi ya leseni kuupa umma ruhusa ya kutumia Toleo Lililobadilishwa chini ya sheria za Leseni, katika mfumo ulioonyeshwa katika kiambatanisho chini.

  7. Hifadhi katika notisi hiyo ya leseni orodha kamili ya Vifungu Visivyoathirika na Nakala za Jalada zinazotakiwa zilizotolewa katika notisi ya leseni ya Nyaraka.

  8. Ongeza nakala isiyobadilishwa ya Leseni hii.

  9. Hifadhi kifungu kiitwacho "Historia", na mada yake, na iongezee kifaa kinachosema japo mada, mwaka, waandishi wapya, na mchapishaji wa Toleo Lililobadilishwa kama ilivyo kwenye Ukurasa wa Mada. Kama hakuna kifungu kiitwacho "Historia" katika Nyaraka, tengeneza moja inayosema mada, mwaka, waandishi, na mchapishaji wa Nyaraka kama ilivyo kwenye Ukurasa wa Mada, kisha ongeza kifaa kinacholelezea Toleo Lililobadilishwa, kama ilivyoelezwa kwenye sentensi iliyopita.

  10. Hifadhi eneo la mtandao, kama lipo, ikiwa katika Nyaraka kwa ajili ya ufikivu wa umma kwenye nakala Wazi ya Nyaraka, na hivyo hivyo maeneo ya mtandao yaliyo kwenye Nyaraka kwa ajili ya matoleo yaliyopita iliyokuwa ikijikita. Hizi zinaweza kuwekwa kwenye kifungu "Historia". Unaweza kuondoa eneo la mtandao kwa kazi ambayo ilichapishwa japo miaka miine kabla ya Nyaraka yenyewe, au mchapishaji halisi wa toleo husika akiruhusu.

  11. Katika kifungu chochote kilichoandikwa "Shukrani" au "Kujitolea", hifadhi mada za vifungu, na hifadhi kwenye vifungu vitu vyote na muonekano wa kila Shukrani ya mchangiaji na/au kujitolea yaliyotolewa.

  12. Hifadhi Vifungu vyote Visivyoathirika vya Nyaraka, bila kubadilishwa nakala na katika sheria zake. Nambari za Vifungu au kinachofanania hazichukuliwi kama sehemu ya kichwa cha kifungu.

  13. Futa kifungu chochote kiitwacho "Idhini". Kifungu kama hicho hakitakiwi kuwepo katika Toleo Lililobadilishwa.

  14. Hutakiwi kukipa upya jina "Idhini" kipengele chochote kilichopo au kuingiliana majina na Kipengele Kisichobadilika chochote.

Kama Toleo Lililobadilishwa linajumuisha vifungu vya mambo ya mbele vipya au viambatanisho ambavyo vina sifa kama Vifungu vya Sekondari na havina kitu chochote kilichonakiliwa kutoka kwenye Nyaraka, unaweza kwa uamuzi wako mwenyewe kuteua baadhi au vifungu vyote hivi kuwa Visivyobadilika. Kufanya hivi, ongeza vichwa vyao vya habari kwenye orodha ya Vifungu Visivyobadilika katika Matoleo Yaliyobadilishwa ya notisi ya leseni. Hivi vichwa vya habari lazima viwe tofauti na vile vya vifungu vingine.

Unaweza kuongeza kipengele kiitwacho "Idhini", ikiwa kwamba haina kitu kingine lakini idhini au uthibitisho wa Toleo Lako jipya kutoka kwa makundi mbali mbali--kwa mfano, kauli ya mapitio ya watu au kwamba nakala imeidhinishwa na shirika au mamlaka ya ufafanuzi wa viwango.

Unaweza kuongeza kifungu cha mpaka maneno matano kama Nakala ya Jalada la Mbele, na kiungu cha mpaka maneno 25 kama Nakala ya Jalada la Nyuma, kwenye mwisho wa orodha ya Nakala za Majalada katika Toleo Lililobadilishwa. Kifungu kimoja tu cha Nakala ya Jalada la Mbele na Nakala ya Jalada la Nyuma kinaweza kuongezwa na (au kupitia mipango iliyofanywa na) chombo chochote kimoja. Kama nyaraka tayari inajumuisha nakala ya jalada kutoka kwenye jalada hilo hilo, iliyoongezwa kabla na wewe au kwa mpango uliofanywa na chombo kile kile ambacho unakitumikia, huwezi kuongeza nyingine; lakini unaweza kuwa mbadala wa lililokuwepo, kwa ruhusa ya wazi kutoka kwa mchapishaji aliyeongeza ya zamani.

Mwandishi (waandishi) na mchapishaji (wachapishaji) wa nyaraka hawatoi ruhus akwa leseni hii kutumia majina yao kwa utangazaji au kwa madai au kama idhini ya Toleo lolote jipya.