KUJUMUISHA NYARAKA

Unaweza kuunganisha Nyaraka hiyo na Nyaraka nyingine zilizotolewa chini ya Leseni hii, chini ya masharti yaliyofafanuliwa katika kifungu 4 juu kwa matoleo yaliyobadilishwa, ikiwa kwamba unajumuisha katika muunganiko Vifungu vyote Visivyoathirika vya nyaraka zote halisi, ambazo hazijabadilishwa, na kuziorodhesha zote kama Vifungu Visivyoathirika vya kazi yako katika notisi yake ya leseni.

Kazi iliyounganishwa inahitaji kuwa na nakala moja ya hii Leseni, na Vifungu Visivyoathirika vingi vinavyofanana vinaweza kubadilishwa na nakala moja. Kama kuna Vifungu Visivyoathirika vingi vyenye jina moja lakini maudhui tofauti, fanya kichwa cha kila kifungu kuwa cha kipekee kwa kuongeza mwishoni mwake, katika mabano, jina la mwandishi halisi au mchapishaji wa kifungu hicho kama anajulikana, au namba ya kipekee. Fanya mabadiliko hayo hayo kwenye vichwa vya vifungu katika orodha ya Vifungu Visivyoathirika kwenye notisi ya leseni ya kazi iliyojumuishwa.

Katika majumuisho, lazima ujumuishe kifungu chochote kilichoandikwa "Historia" katika nyaraka halisi zozote, kutengeneza kifungu kimoja kiitwacho "Historia"; hivyo hivyo jumuisha vifungu vyovyote viitwavyo "Shukrani", na vifungu vyovyote viitwavyo "Kujitolea." Lazima ufute vifungu vyote viitwavyo "Endorsements."