Unaweza kutengeneza mkusanyiko unaojumuisha Nyaraka hiyo na nyaraka nyingine zilizotolewa chini ya Leseni hii, na kubadilisha nakala binafsi za leseni hii katika nyaraka tofauti kwa kutumia nakala moja ambayo imejumuishwa na mkusanyiko huu, ikiwa kwamba unafuata sheria za Leseni hii, kwa kunakili bila mabadiliko katika kila nyaraka kwa mambo mengine yote.
Unaweza kutoa dondoo ya nyaraka moja kutoka kwenye mkusanyiko, na kuisambaza kibinafsi chini ya hii Leseni, ikiwa umeingiza nakala ya leseni hii kwenye nyaraka hiyo, na kufuata hii Leseni katika mambo mengine yote kuhusu kunakili bila mabadiliko ya nyaraka hiyo.