MAREKEBISHO YA BAADAYE YA HII LESENI

Free Software Foundation inaweza kuchapisha toleo jipya, lililorekebishwa la GNU Free Documentation Licence kutoka muda hadi muda. Matoleo hayo mapya yatakuwa sawa kiroho na toleo la sasa, lakini yanaweza kutofautiana kiundani kushughulikia matatizo mapya au wasiwasi. Tembelea http://www.gnu.org/copyleft/.

Kila toleo la Leseni limepewa nambari ya toleo tofauti na nyingine. Kama nyaraka ikibainisha kwamba toleo la Leseni hii lenye nambari fulani "au toleo lolote la mbele" linahusika nayo, una machaguo ya kufuata masharti na vigezo ya aidha toleo lililobainishwa au toleo lolote la mbele ambalo limechapishwa (sio kama rasimu) na Free Software Foundation. Kama nyaraka haijabainisha nambari ya toleo la hii Leseni, unaweza kuchagua toleo lolote lilillowahi kuchapishwa (sio kama rasimu) na Free Software Foundation.