Jinsi ya kutumia hii Leseni kwa ajili ya nyaraka zako

Kutumia hii leseni kwenye nyaraka uliyoandika, jumuisha nakala ya Leseni kwenye nyaraka na weka hakimiliki ifuatayo na notisi za leseni baada tu ya ukurasa wa mbele:

Hakimiliki (c) JINA LAKO. Ruhusa imetolewa kunakili, kusambaza na/au kurekebisha nyaraka hii chini ya masharti ya GNU Free Documentation Licence, Toleo 1.1 au toleo lolote la mbele lililochapishwa na Free Software Foundation; na sehemu zisizobadilika zikiwa ORODHESHA VICHWA VYA HABARI VYAO, na Nakala za Jalada la Mbele likiwa ORODHA, na Jalada la Nyuma likiwa ORODHA. Nakala ya leseni imejumuishwa katika kifungu kiitwacho "GNU Free documentation Licence" .

Kama hauna Vifungu Visivyobadilika, andika "bila Vifungu Visivyobadilika" badala ya kusema ni vipi havibadiliki. Kama hauna Nakala za Jalada la Mbele, andika "hakuna Nakala za Jalada la Mbele" badala ya "Nakala za Jalada la Mbele kuwa ORODHA"; hivyo hivyo kwa Nakala za Jalada la Nyuma.

Kama nyaraka yako ina mifano iliyo ya msingi ya kanuni za programu, tunashauri kutoa hii mifano sambamba chini ya leseni huru ya programu ya chaguo lako, kama GNU General Public License, kuruhusu utumizi wake katika programu za bure.