Tafsiri inachukuliwa kama aina ya ubadilishaji, kwa hiyo unaweza kusambaza tafsiri ya Nyaraka chini ya masharti ya kifungu 4. Kubadilisha Vifungu Visivyobadilika kwa tafsiri inahitaji ruhusa maalumu kutoka kwa wanaoshikilia hakimiliki, lakini unaweza kujumuisha tafsiri ya baadhi au Vifungu Visivyobadilika vyote, kama nyongeza kwa matoleo halisi ya hivi Vifungu Visivyobadilika. Unaweza kujumuisha tafsiri ya hii Leseni ikiwa kwamba umejumuisha pia toleo halisi la Kiingereza la hii Leseni. Ikitokea kutokuwapo na makubaliano kati ya tafsiri na toleo halisi la Kiingereza la hii Leseni, toleo halisi la Kiingereza litatumika.