Baadhi ya kazi katika OTRS, kama upandishaji na kufungua kiotomatiki tiketi, inategemea kwenye usanidi sahihi wa masaa ya biashara, majira ya saa na sikukuu. Unaweza kufafanua hii kupitia Kiolesura cha SysConfig, katika Kiunzi > Kiini::Muda. Unaweza kuweka bayana seti tofauti za masaa ya kazi, sikukuu na majira ya saa kama 'Kalenda' tofauti katika Kiunzi > Kiini::Muda::Kalenda1 kupitia Kiunzi > Kiini::Muda::Kalenda9. Kalenda zinaweza kufafanuliwa na mipangilio ya foleni, au ngazi za SLA. Hii ina maanisha, kwa mfano, unaweza kuweka bayana kalenda yenye masaa ya biashara 5 x 8 kwa SLA yako ya 'Kawaida', lakini ukatengeneza kalenda tofauti ya msaada wa 7 x 24 kwa SLA zako za 'dhahabu'; na pia kuseti kalenda kwa ajili ya foleni yako ya 'Msaada-USA' yenye dirisha tofauti la muda tofauti na lile la foleni yako ya 'Msaada-Japan'. OTRS inaweza kushughulikia mpaka kalenda tofauti 99.
Seti masaa ya kazi kwa ajili ya mfumo wako katika SysConfig kiunzi> Kiini::Muda::MudaMasaaYaKazi, au kwa kalenda zako maalumu katika usanidi wa kalenda. OTRS inaweza kushughulikia muda wa saa moja. Kuweka alama katika visanduku 8, 9, 10 ... 17 inaendana na masaa ya kazi ya 8 asubuhi - 6 alasiri.
Katika masaa ya biashara tu ndio tiketi zinaweza kupanda, taarifa za tiketi zilizopandishwa na tiketi zinazosubiri zinatumwa, na tiketi zinafunguliwa.
Sikukuu ambazo ziko kwenye tarehe funge kila mwaka, kama Mwaka mpya au tarehe nne ya Julai, zinaweza kubainishwa katika MudaSikukuuSiku, au katika sehemu husika kwa ajili ya kalenda 1-9
Tiketi hazitapandishwa wala kufunguliwa katika siku zilizofafanuliwa kama MudaSikuZaSikukuu.
Kwa chaguo-msingi OTRS inasafirishwa na sikukuu za German zimesakinishwa.
Sikuku kama Pasaka ambazo hazima tarehe maalumu ya mwaka lakini badala yake zinabadilika kila mwaka, zinaweza kubainishwa kwenye MudaSikuZaSikukuuMaraMoja.
Tiketi hazitapandishwa na hazitafunguliwa katika tarehe zilizofafanuliwa katika MudaSikuZaSikukuuMaraMoja
OTRS haisafirishwi na sikukuu yoyote ya Wakati-Mmoja ikiwa imesakinishwa. Hii ina maanisha unatakiwa kuongeza sikukuu, kama Pasaka au Sikuku ya Shukrani, kwenye mfumo wakati wa kusanidi OTRS.
Tiketi zilizofungwa zinaweza kufunguliwa kiotomatiki na mfumo. Hiki kipengele kinaweza kuwa cha muhimu, kwa mfano, wakala amefunga tiketi ambazo zinatakiwa kuchakatishwa, lakini hawezi kuzifanyia kazi kwa sababu fulani, tuseme yuko nje ya ofisi kwa dharura. Kipengele otomatiki cha kufungua kinafungua tiketi baada ya muda fulani kuhakikisha hakuna tiketi zilizofungwa zitakazosahaulika, hivyo kuruhusu mawakala wengine kuzichakatisha.
Idadi ya muda kabla tiketi haijafunguliwa inaweza kuwekwa bayana katika
mipangilio ya foleni kwa kila
foleni. Moduli bin/otrs.UnlockTickets.pl
, ambayo
inatekelezwa kwa kipindi fulani kama kazi ya mfumo iliyopangwa, inafanya
ufunguaji otomatiki wa tiketi.
Taarifa kuhusu tiketi zilizofunguliwa zinatumwa nje kwa wale mawakala wenye foleni zilizosetiwa tiketi zilizofunguliwa kwenye 'Foleni zangu', na wame amilisha taarifa kwenye tiketi zilizofunguliwa katika mapendeleo yao binafsi.
Tiketi zitafunguliwa kama masharti yote yafuatayo yamefikiwa:
Kuna muda wa mwisho wa kufungua umefafanuliwa kwenye foleni ambayo tiketi imo.
Tiketi imesetiwa kuwa imefungwa.
Hali ya tiketi ni wazi.
Muda wa kufungua utasetiwa upya kama wakala akiongeza makala mpya ya nje kwenye tiketi. Inaweza kuwa ya aina yoyote kati ya zifuatazo: barua pepe-nje, simu, faksi, sms, au notisi-nje.
Pia, kama makala ya mwisho katika tiketi imetengenezwa na wakala, na mteja akaongeza nyingine, aidha kwa kupitia majibu ya tovuti au barua pepe, muda wa kufungua utasetiwa upya.
Tukio la mwisho ambalo lita seti upya muda wa kufungua ni pale tiketi imegawiwa kwa wakala mwingine.