Usanidi wa Mfumo

Mafaili ua usanidi wa OTRS
Usanidi wa mfumo kupitia kiolesura cha mtandao

Mafaili ua usanidi wa OTRS

Mafaili yote ya usanidi ya OTRS yanahifadhiwa katika mpangilio orodha Kernel na katika sehemu zake ndogo. Hakuna haja ya kubadilisha kwa mikono faili jingine zaidi ya Kernel/Config.pm, kwa sababu mafaili yaliyobaki yatabadilishwa mfumo ukiboreshwa. Nakili parameta za usanidi kutoka mafaili mengine kwenda Kernel/Config.pm na zibadilishe kutegemeana na mahitaji yako. Hili faili halitaguswa wakati wa mchakato wa kuboreshwa, kwahiyo mipangilio yako ya mikono iko salama.

Katika mpangilio orodha Kernel/Config/Files kuna mafaili mengine ambayo yanachanganuliwa wakati kurasa ya kuigia ya OTRS inafikiwa. Kama programu-tumizi za ziada kama Maswali yanayoulizwa mara kwa mara au Meneja Mafaili zimesakinishwa, mafaili ya usanidi ya hizi pia yanaweza kupatikana katika njia iliyotajwa.

Kama kiolesura cha tovuti cha OTRS kimefikiwa, mafaili yote ya .xml katika mpangilio orodha wa Kernel/Config/Files yanachanganuliwa katika mpangilio wa alfabeti, na mipangilio ya kiunzi cha kati na programu-tumizi za ziada zitapakiwa. Baada ya hapo, mipangilio ya kwenye mafaili Kernel/Config/Files/ZZZAAuto.pm, Kernel/Config/Files/ZZZAuto.pm na Kernel/Config/Files/ZZZProcessManagement.pm (kama lipo) yata tathminiwa. Haya mafaili yanatumiwa na kiolesura michoro kwa ajili ya kuhifadhi kwa muda usanidi wa mfumo na hayatakiwi kubadilishwa kwa mikono kamwe. Mwisho, faili Kernel/Config.pm lenye mipangilio yako na parameta zilizobadilishwa kwa mikono, litachanganuliwa. Kusoma mafaili ya usanidi kwa mpangilio huu inahakikisha kwamba mipangilio yako maalumu inatumiwa na mfumo.

Usanidi wa mfumo kupitia kiolesura cha mtandao

Tangu OTRS 2.0, karibu parameta zote za usanidi za kiunzi cha kati au vya programu-tumizi za ziada zilizosakinishwa, zinaweza kubadilishwa kirahisi na kiolesura michoro cha mfumo. Ingia kama msimamizi wa OTRS na fuata kiungo cha SysConfig katika kurasa ya Msimamizi kutekeleza kifaa kipya cha usanidi (ona Kielelezo chini).

Kielelezo: Kiolesura mchoro cha usanidi wa mfumo.

OTRS kwa sasa ina zaidi ya parameta za usanidi 600, na kuna njia tofauti za kufikia kila moja kirahisi. Kwa utafutaji wa nakala kamili, parameta zote za usanidi zinaweza kutafutwa kwa kutumia herufi moja au mbili za muhimu. Utafutaji wa nakala huru hautafuti tu kwenye majina ya parameta za usanidi, bali pia kwenye maelezo ya parameta. Hii inafanya elementi kupatikana kirahisi hata kama jina lake halijulikani.

Kwa zaidi, parameta zote za usanidi zinapangwa katika makundi muhimu na makundi madogo. Makundi muhimu yanawakilisha programu-tumizi ambazo parameta za usanidi zipo ndani yake, mf. "Kiunzi" kwa ajili ya kiunzi cha kati cha OTRS, "Tiketi" kwa ajili ya mfumo wa tiketi, "Maswali yanayoulizwa Mara kwa Mara" kwa ajili ya mfumo wa Maswali yanayoulizwa Mara kwa Mara, na kadhalika. Makundi madogo yanaweza kufikiwa kama programu-tumizi imechaguliwa kutoka kwenye boksi la orodha ya makundi na kitufe cha "Chagua kundi" kimebonyezwa.

Kila parameta ya usanidi inaweza kuwashwa au kuzimwa kwa kupitia kisanduku tiki. Kama parameta imezimwa, mfumo utapuuza hii parameta au kutumia chaguo-msingi. Inawezekana kurudisha parameta ya usanidi iliyobadilishwa kuwa chaguo-msingi la mfumo kwa kutumia kiungo cha kuseti upya. Kitufe cha Kusasisha kinawasilisha mabadiliko yote kwenye parameta za usanidi wa mfumo.

Kama unataka kuhifadhi mabadiiko yote uliyofanya kwenye usanidi wa mfumo wako, kuanzisha usakinishaji mpya kwa haraka, unaweza utumia kitufe "Hamisha mipangilio", ambacho kitatengeneza faili la .pm. Kurudisha mipangilio yako, bonyeza "Agiza mipangilio" na chagua .pm iliyotengenezwa kabla.

Note

Kwa sababu za kiusalama, parameta za usanidi wa miunganiko ya hifadhidata haziwezi kubadilishwa katika kifungu SysConfig. Inabidi zisetiwe kwa mikono katika Kernel/Config.pm.