Hii sura inaelezea chelezo na urejeshaji wa data za OTRS.
Kuna aina mbili za data za kuweka kwenye chelezo: mafaili ya programu-tumizi
(mf. mafaili ya kwenye /opt/otrs
), na data
zilizohifadhiwa kwenye hifadhidata.
Kurahisisa chelezo, hati scripts/backup.pl
imejumuishwa
katika kila usakinishaji wa OTRS. Inaweza kuanzishwa ili kuweka chelezo la
kila data muhimu (ona Hati chini).
linux:/opt/otrs# cd scripts/ linux:/opt/otrs/scripts# ./backup.pl --help backup.pl - backup script Copyright (C) 2001-2018 OTRS AG, https://otrs.com/ usage: backup.pl -d /data_backup_dir/ [-c gzip|bzip2] [-r 30] [-t fullbackup|nofullbackup|dbonly] linux:/opt/otrs/scripts#
Hati: Kupata usaidizi wa utaratibu wa chelezo la OTRS.
Tekeleza amri zilizowekwa bayana kwenye hati hapo chini kutengeneza chelezo:
linux:/opt/otrs/scripts# ./backup.pl -d /backup/ Backup /backup//2010-09-07_14-28/Config.tar.gz ... done Backup /backup//2010-09-07_14-28/Application.tar.gz ... done Dump MySQL rdbms ... done Compress SQL-file... done linux:/opt/otrs/scripts#
Hati: Kutengeneza chelezo.
Data zote zimehifadhiwa kwenye mpangilio orodha
/chelezo/2010-09-07_14-28/
(ona hati hapo chini). Kwa
zaidi, data zilihifadhiwa kwenye faili la .tar.gz
linux:/opt/otrs/scripts# ls /backup/2010-09-07_14-28/ Application.tar.gz Config.tar.gz DatabaseBackup.sql.gz linux:/opt/otrs/scripts#
Hati: Kukagua mafaili ya chelezo.
Kurejesha chelezo, data zilizohifadhiwa za programu-tumizi zina andikwa upya
kwenye mpangilio orodha wa usanikishaji,
mf. /opt/otrs
. Pia hifadhidata inabidi irejeshwe.
Hati hati/rejesha.pl
(ona hati chini), ambayo
inarahisisha mchakato wa kurejesha, inasambazwa na kila usanikishaji wa
OTRS. Ina usaidizi kwa MySQL na PostgreSQL.
linux:/opt/otrs/scripts# ./restore.pl --help restore.pl - restore script Copyright (C) 2001-2018 OTRS AG, https://otrs.com/ usage: restore.pl -b /data_backup/<TIME>/ -d /opt/otrs/ linux:/opt/otrs/scripts#
Hati: Kupata usaidizi wa utaratibu wa urejeshaji.
Data ambazo zimehifadhiwa, kwa mfano, kwenye mpangilio orodha
/chelezo/2010-09-07_14-28/
, inaweza kurejeshwa na amri
zilizo kwenye hati hapa chini, kwa kuamini usanikishaji wa OTRS upo kwenye
/opt/otrs
.
linux:/opt/otrs/scripts# ./restore.pl -b /backup/2010-09-07_14-28 -d /opt/otrs/ Restore /backup/2010-09-07_14-28//Config.tar.gz ... Restore /backup/2010-09-07_14-28//Application.tar.gz ... create MySQL decompresses SQL-file ... cat SQL-file into MySQL database compress SQL-file... linux:/opt/otrs/scripts#
Hati: Kurejesha data za OTRS .