Hiki kifungu kinashughulikia machaguo yanayoweza kusanidiwa kwa ajili ya matokeo ya PDF kwenye OTRS.
Kama ukitumia kitendo cha Kuchapisha kutoka kokote ndani ya kiolesura cha OTRS, itazalisha faili lililoumbuizwa la PDF. Unaweza kulemaza hii kwa kubadilisha usanidi wa parameta PDF kutengeneza HTML badala yake.
Unaweza kurekebisha muonekano wa mafaili yanayozalishwa na OTRS kwa kutengeneza nembo yako na kuiongeza kwenye PDF::FailiLaNembo. Unaweza kutumia PDF::UkubwaWaKurasa kufafanua ukubwa wa kawaida wa faili la pdf linalozalishwa (DIN-A4 au barua), na pia PDF::KikomoKurasa kuweka bayana idadi ya kikomo cha juu cha kurasa kwa faili la pdf, ambayo ni muhimu kama mtumiaji akizalisha faili kubwa kwa makosa.
Moduli za Perl CPAN za PDF::API2 na Compress::Zlib lazima zisakinishwe kwa ajili ya uzalishaji wa mafaili ya pdf. Katika usambazaji mwingi zinapatikana kama vifurushi na vinaweza kusakinishwa kirahisi, kwa kutumia meneja kifurushi husika. Ikiwa hii haiwezekani, inabidi zisakinishwe na CPAN. Kwa taarifa zaidi kuhusu kusakinisha moduli za Perl, tafadhali pitia kifungu cha "Usakinishaji wa moduli za Perl".