Moduli ya takwimu ya OTRS inashikilia sifa za kufuatilia takwimu za operesheni na inazalisha ripoti zake yenyewe zinazohusiana na matumizi ya OTRS. Mfumo wa OTRS unatumia msemo "stat" kwa ujumla kumaanisha ripoti inayowakilisha viashiria mbali mbali.
Usanidi sahihi wa moduli ya takwimu ya OTRS unahusika na wingi wa mahitaji na mapendeleo. Hii inajumuisha moduli mbali mbali za kutathminiwa, mipangilio ya ruhusa za mtumiaji, viashirio kupigiwa hesabu na ngazi za ugumu, urahisi wa usanidi wa moduli za takwimu, kasi na ufanisi wa mahesabu, na msaada kwa seti tajiri za lahaja zinazotoka.
Elementi za takwimu, mafaili yanayoongeza kazi za moduli ya takwimu kwa mahitaji fulani, yanaweza kuunganishwa kutafuta thamani ya takwimu changamano.
Ukiingia kama wakala, mwambaa wa uabiri otaonyesha kiungo "Takwimu", na machaguo ya menyu ndogo tofauti tofauti, kama ilivyoonyeshwa kwenye Kielelezo.
Kielelezo: Machaguo ya menyu ya takwimu.
Machaguo tofauti yanayotolewa katika menyu ya takwimu ni:
Mapitio. Inawasilisha orodha ya ripoti tofauti zilizosanidiwa kabla.
Mpya. Inahitaji haki za kusoma na kuandika.
Agiza. Inahitaji haki za kusoma na kuandika.
Kwa kuchagua kiungo cha "Takwimu" kwenye mwambaa wa uabiri, na kisha kiungo cha menyu ndogo "Mapitio", inaita skrini ya Mapitio. Skrini ya mapitio inaonyesha orodha ya ripoti zote ambazo zimesanidiwa kabla na wakala anaweza kutumia (ona Kielelezo chini).
Kielelezo: Mapitio ya ripoti za kawaida.
Taarifa ifuatayo inatolewa kwa kila ripoti ya kawaida iliyoorodheshwa kwenye Mapitio:
Takwimu#. Namba ya ripoti ya kipekee.
Kichwa. Kichwa cha ripoti.
Kitu. Kitu kinachotumika kuzalisha takwimu. Katika kesi ya takwimu tuli, hakuna kitu kinachoonyeshwa kwa kuwa hakuna kitu kinachobadilika kinachotumika kwa uzalishaji wake.
Maelezo. Maelezo mafupi ya ripoti.
Wakati moduli ya takwimu imesakinishwa, inakuja na ripoti chache za mfano zilizoagizwa kwenye mfumo. Hizi zinaonyeshwa kama orodha kwenye kurasa ya Mapitio. Kama kurasa ya mapitio ikipanuliwa kuwa zaidi ya kurasa moja, wakala anaweza kuvinjari kwenye kurasa tofauti. Orodha ya ripoti inaweza kupangwa unavyotaka, kwa kubofya kichwa cha safuwima unayotaka katika orodha. Kuzalisha ripoti maalumu, bofya kwenye nambari ya takwimu inayohusika na ripoti katika orodha ya Mapitio. Hii inaleta kiolesura "Muonekano" cha ripoti.
Kiolesura cha muonekano wa mtumiaji inatoa mipangilio ya usanidi wa takwimu. (ona Kielelezo chini).
Kielelezo: Kuona ripoti maalumu.
Mipangilio ya usanidi wa ripoti fulani inaweza kusetiwa ndani ya machaguo mbali mbali kwenye skrini ya kuona. Aidha mtengenezaji wa ripoti au mtu mwingine yoyote mwenye ruhusa zinazotakiwa anaweza kuweka mipangilio.
Kurasa inaonyesha vifuatavyo:
Vitendo viwezekanavyo:
Nenda kwenye mapitio. Kiungo kinakurudisha kwenye orodha ya mapitio ya ripoti.
Hariri. Hariri muundo wa ripoti ya sasa (haki za kusoma na kuandika zinahitajika).
Futa. Futa ripoti ya sasa (haki za kusoma na kuandika zinahitajika).
Hamisha usanidi. Hamisha ripoti ya usanidi, kupitia upakuaji wa faili (haki za kusoma na kuandika zinahitajika)
Matumizi: Fomula saidizi za Agiza na Hamisha zinaruhusu kwa urahisi wa kutengeneza na kujaribu ripoti katika mifumo ya majaribio na urahisi wa kuingiza kwenye mfumo wa uzalishaji.
Undani wa ripoti:
Takwimu#. Nambari ya ripoti.
Kichwa. Kichwa cha ripoti.
Kitu. Kitu kinachotumika kutengeneza ripoti.
Maelezo. Maelezo ya dhumuni la ripoti.
Umbizo. Umbizo la ripoti itakayotoka, inategemea na usanidi, inaweza kuwa mojawapo ya maumbizo yafuatayo:
CSV.
Chapisha
Grafu-mistari
Grafu-miambaa.
Grafu-miambaa h.
Grafu-pointi.
Grafu-mistari-pointi.
Grafu-eneo.
Grafu-duara.
Ukubwawagrafu. Ukubwa katika pikseli kwa ajili ya mchoro / chati. Hili chaguo linatolewa pale tu usanidi wa ripoti unaruhusu chati. Ukubwa wowowte unaoweza kutumika kwa ujumla unasaniwa na msimamizi wa OTRS kwenye SysConfig. Wakala kisha anaweza kuchagua kabla umbizo husika, wakati anasanidi ripoti.
Jumla safumlalo. Inaonyesha kama ripoti imerekebishwa kwa safuwima, ambamo seli zake zinatoa jumla ya safumlalo husika.
Jumla safuwima. Inaonyesha kama ripoti imerekebishwa kwa safumlalo, ambamo seli zake zinatoa jumla ya safuwima husika.
Hifadhi muda. Inaonyesha kama ripoti iliyozalishwa inawekwa kwenye hifadhi muda ya mfumo.
Halali. Hii inaweza kusetiwa kuwa "batili" kama ripoti itatakiwa kuanzishwa kwa muda kwa sababu yoyote. Kitufe "Anza" upande wa chini wa paneli ya kulia haionyeshwi tena. Ripoti haiwezi kuzalishwa tena.
Tengenezwa. Muda wa utengenezaji wa ripoti.
Imetengenezwa na. Jina la wakala aliyetengeneza ripoti.
Badilishwa. Muda ripoti ilibadilishwa kwa mara ya mwisho.
Imabadilishwa na. Jina la wakala aliyebadilisha ripoti mara ya mwisho.
jira-X. Kutumia programu-tumizi hii, wakala anaweza kubadilisha majira x na y (ikiwa tu imeamilishwa na msimamizi wa OTRS).
Taarifa ya ujumla inafwatiwa na taarifa kuhusu ripoti yenyewe. Kuna muonekano wa ripoti (au takwimu) wa aina mbili :
Muonekano tuli wa takwimu. Vizalishaji vya ripoti tuli vinaweza kuunganishwa katika moduli ya takwimu (ona Kielelezo chini).
Kielelezo: Kuona ripoti tuli.
Muonekano wa takwimu unaobadilika (ona Kielelezo juu). Zinaweza kuonyeshwa katika njia mbili:
Mipangilio isiyobadilika. Chanzo cha ripoti hakina ruhusa ya kubadilisha hizi sehemu.
Mipangilio inayobadilika. Mipangilio ya usanidi wa ripoti kama hizi inaweza kubadilishwa na wakala.
Kubonyeza kitufe "Anza" (upande wa chini wa skrini) ni hatua ya mwisho ya kuzalisha ripoti. Kuna njia mbili ziwezekanazo kwa hiki kitufe kuto kuonyeshwa:
Ripoti imesetiwa kuwa batili na hivyo imelemazwa.
Ripoti haikufanyiwa usanidi vizuri, hivyo haiwezi kutekelezeka. Kwa kesi hii taarifa zinazotakiwa zinapatikana katika sehemu ya taarifa za OTRS (chini kuna mwambaa wa uabiri).
Kama mpangilio kwenye Ona kurasa hauko sawa, hii kurasa itaonyeshwa tena baada ya kubonyeza kitufe "Anza", na taarifa kuhusu ingizo lipi limekosewa zitatolewa kwenye sehemu ya taarifa.
Mawakala wenye haki za kuandika wanaweza kuhariri usanidi wa ripoti kwa kuita kiolesura cha hariri mtumiaji cha moduli ya takwimu. Au, wanaweza kutengeneza ripoti mpya. Skrini zinazohusika zinaweza kufikiwa kwa njia zifuatazo:
Hariri: Kupitia kitufe cha "Hariri" kwenye muonekano wa takwimu.
Mpya: Kupitia kiungo "Mpya" kwenye menyu sa takwimu kutoka kwenye mwambaa wa uabiri, au kitufe cha "Ongeza" kutoka kwenye kurasa ya Mapitio.
Takwimu zina haririwa na sogora katika hatua nne:
Ubainishaji wa jumla.
Fasili ya elementi kwa ajili ya jira-X.
Ubainishaji wa thamani za mfuatano.
Kuchagua vizuizi kuweka kikomo kwenye ripoti.
Hatua 2 kupitia 4 zinahitajika tu kwa uzalishaji wa ripoti zenye takwimu zinazobadilika. Kwa takwimu tuli, taarifa za ujumla tu (pointi 1) ndio zinahitajika.
Taarifa kuhusu jinsi ya kushughulikia ukurasa inatolewa katika kila skrini, chini ya paneli ya Vitendo katika paneli ya madokezo.
Kama maingizo yasiyo sahihi yameingizwa, kiolesura kilichopita kilichochakatishwa kitaonyeshwa tena na kitakuwa na taarifa kuhusu maingizo yasiyosahihi. Hii taarifa inaweza kupatikana katika kifungu cha taarifa cha OTRS. Kiolesura cha maingizo cha mtumiaji kinachofwata kinaonyeshwa tu baada ya fomu ya sasa kujazwa kwa usahihi.
Ubainishaji wa jumla. Ni kurasa ya kwanza ya Hariri sogora (ona Kielelezo chini).
Kielelezo: Kuhariri ubainishaji wa jumla wa ripoti.
Kwenye skrini iliyoonyeshwa kwenye Kielelezo, kuna idadi kubwa ya vipimo na mipangilio ambayo inaweza kuhaririwa:
Mada. Inatakiwa iakisi lengo la takwimu kwa ufupi..
Maelezo. Maelezo zaidi ya taarifa kuhusu ufafanuzi wa ripoti, aina ya parameta za usanidi, na kadhalika.
KItu kinachobadilika. Kama usanikishaji wa OTRS utatoa vitu vinavyobadilika vingi, mojawapo inaweza kuchaguliwa. Hivi vitu vinafikia mahitaji ya moduli fulani.
Faili tuli. Kwa kawaida chaguo hili halionyeshwi, kwakuwa mafaili tuli ambayo bado hayaja gawiwa kwa ripoti yoyote ndiyo yanayoonyeshwa tu. Hata hivyo kama "Faili tuli" limeonyeshwa, ni muhimu kuweka alama ya pata kwenye sehemu ya chaguo na kuchagua njia ya uzalishaji (inayobadilika na kitu kinachobadilika au tuli na faili). Kama faili tuli limechaguliwa, violesura vya maingizo 2 mpaka 4 havionyeshwi kwa kuwa faili tuli lina mipangilio yote inayotakiwa.
Mipangilio ya ruhusa. Kuwezesha vizuizi vya makundi (na hivyo mawakala) ambao baadaye wanaweza kuona na kuzalisha ripoti zilizosanidiwa. Hivyo ripoti mbali mbali zinaweza kutengewa idara tofauti na makundi ya kazi yanazozihitaji. Inawezekana kutengea ripoti moja kwa makundi tofauti.
Mfano 1: Kundi la "takwimu" lilichaguliwa. Ripoti inaonekana kwa watumiaji wote wenye japo haki za kusoma tu kwenye kundi la "takwimu". Huu ufikivu upo kwa chaguo-msingi.
Mfano 2: Kundi liitwalo "mauzo" lilichaguliwa. Watumiaji wenye haki ya kusoma tu ya kundi "mauzo" wanaweza kuona takwimu katika hali-tumizi ya muonekano na kuizalisha. Hata hivyo, ripoti haitakuwepo kwa ajili ya kuangaliwa na watumiaji wengine.
Umbizo. Umbizo la matokeo ya takwimu: Kutegemeana na usanidi, kati ya maumbizo yafuatayo yanaweza kuchaguliwa:
CSV.
Chapisha
grafu-mistari.
grafu-miambaa.
grafu-miambaa h
grafu-pointi.
grafu-mistari-pointi.
grafu-eneo.
grafu-duara.
Ukubwawagrafu. Chagua ukubwa wa chati katika pikseli. Huu uchaguzi ni muhimu kama umbizo la matokeo ya mchoro limechaguliwa chini ya "Umbizo". Ukubwa wa aina zote wa grafu ambao unaweza kutumiwa kwa ujumla unafafanuliwa na msimamizi wa OTRS katika SysConfig. Wakati wa kusanidi ripoti, wakala anaweza kuchagua kabla ma umbizo yote yanayo husika.
Jumla safumlalo. Inaonyesha kama ripoti imerekebishwa kwa safuwima, ambamo seli zake zinatoa jumla ya safumlalo husika.
Jumla safuwima. Inaonyesha kama ripoti imerekebishwa kwa safumlalo, ambamo seli zake zinatoa jumla ya safuwima husika.
Hifadhi muda. Inabainisha kama ripoti iliyozalishwa inatakiwa kuwekwa kwenye hifadhi muda ndani ya mfumo wa mafaili. Hii inaokoa nguvu na muda wa michakato ya kompyuta kama ripoti ikiitwa tena, lakini inatakiwa itumike tu kama maudhui ya ripoti hayabadiliki tena.
Kuweka kwenye hifadhi muda kunazuiwa kama ripoti haina thamani zinazowajibika za muda, au thamani zinazowajibika za muda zinaashiria mbeleni.
Kama ripoti iliyo kwenye hifadhi muda imehaririwa, data zote za kwenye hifadhimuda zinafutwa.
Halali. Hii inaweza kusetiwa kuwa "batili" kama ripoti iliyosanidiwa kabla haitakiwi kuanzishwa kwa muda kwa sababu yoyote. Kitufe cha "Anza" upande wa chini wa paneli y akulia haionyeshwi tena. Ripoti haiwezi kuzalishwa tena.
Fasili ya elementi kwa ajili ya jira-X. Ni usanidi wa elementi unaotumika kwa ajili ya uwakilishaji wa jira-X au, kama majedwali yametumika, ya jina la safuwima linalotumika kwenye jira-X (ona Kielelezo) .
Kielelezo: Fasili ya elemnti kwa ajili ya jira-X.
Kwanza kabisa, elementi inachaguliwa kwa kutumia sehemu ya chaguo. Kisha sifa mbili au zaidi za elementi lazima zichaguliwe. Kama hakuna sifa zilizochaguliwa, sida zote zinatumika kujumuisha zile zilizoongezwa baada ya usanidi wa ripoti.
Kama mipangilio "Funge" imelemazwa, wakala anayezalisha ripoti anaweza kubadilisha sifa za elementi husika katika kiolesura cha "Muonekano".
Elementi za muda ni tofauti kwa kuwa kipindi cha muda na skeli lazima vijaribiwe. Aina na idadi ya matokeo ya elementi kutoka kwenye kitu kinachobadilika kilichotumika na kubadilika kwa kukitegemea.
Kama ingizo si sahihi, kitufe "Inayofwata" kinaelekeza kwenye mfumo wa "Thamani za mfuatano". Pia inawezekana kurudi nyuma kuhariri vifungu vya mwanzoni.
Ubainishaji wa mfuatano wa thamani.
Katika hatua ya tatu ya usanidi wa ripoti, thamani za mfuatano zinafafanuliwa (ona Kielelezo chini). Baadaye zitatengeneza grafu binafsi au misururu mbali mbali ndani ya muonekano wa jedwali
Kielelezo: Ufafanuzi wa thamani za mfuatano.
Kama elementi imechaguliwa, kila sifa itakayochaguliwa itahusiana na thamani ya mfuatano (ona Mfano 19-1 chini).
Example 4.19. Ufafanuzi wa thamani ya mfuatano - elementi moja
Elementi Foleni:
Thamani za mfuatano 1 = Mbichi
Thamani za mfuatano 2 = Taka
....
Kama elementi mbili zimechaguliwa, kila sifa iliyochaguliwa ya elementi ya kwanza inaunganishwa na sifa ya elementi ya pili kutengeneza thamani za mfuatano (ona Mfano 19-2 chini).
Example 4.20. Ufafanuzi wa thamani za mfuatano - elementi mbili
Elementi 1 foleni, Elementi 2 hali:
Thamani za mnyororo 1 = Mbichi - wazi
Thamani za mfuatano 2 = Mbichi - imefungwa kwa mafanikio
Thamani za mfuatano 3 = Taka - wazi
Thamani za mfuatano 4 = Taka - imefungwa kwa mafanikio
Uchaguzi wa elementi tatu au zaidi hauruhusiwi.
Kwa nyongeza masharti hayo hayo yanafanya kazi kwa uchaguzi wa sifa na kisanduku tiki "Funge" na pia kwenye uchaguzi wa "jira-X":
Kama hakuna sifa za elementi zilizochaguliwa, sifa zote zitatumika, ikijumuisha zile zilizo ongezwa baada ya ripoti ya usanidi.
Kama mpangilio "Funge" umelemazwa, wakala anaezalisha ripoti anaweza kubadilisha sifa za elementi husika.
Kuweka vizuizi kwenye ripoti. Hii ni hatua ya nne na ya mwisho ya usanidi (ona Kielelezo chini). Vizuizi vinasaidia kuweka kikomo cha matokeo kwa vigezo vilivyochaguliwa. Katika kesi nyingi, hakuna vizuizi vya kuwekwa kabisa.
Kielelezo: Fasili ya vizuizi.
Baada ya vizuizi vyote kusetiwa, usanidi wa ripoti unamalizika kwa kubonyeza kitufe "Maliza".
Kiolesura cha Agiza mtumiaji (ona Kielelezo chini) kinaweza kufikiwa kwa kuchagua kutoka kwenye mwambaa wa uabiri, kiungo "Takwimu", kisha "Agiza". Pia, kubonyeza kitufe cha Agiza katika skrini ya Mapitio inaleta matokeo sawa. Haki za "kusoma na kuandika"kwenye ripoti zinatakiwa.
Kielelezo: Kiolesura cha Kuagiza mtumiaji.
Inarahisisha uagizaji wa ripoti na ni, pale inapounganishwa na fomula saidizi hamisha ya moduli, fomula saidizi muhimu sana. Takwimu zinaweza kutengenezwa na kujaribiwa kirahisi kwenye mifumo ya majaribio, kisha kuagizwa nakuingia kwenye mfumo wa uzalishaji.
Uagizaji unaathiriwa na kupakia faili. Kiolesura cha "Ona" cha ripoti iliyoagizwa kinafunguliwa kiotomatiki baada ya hapo.
Hii sehemu inatoa maelezo kuhusu kazi na majukumu ya Msimamizi wa OTRS anayehusika na moduli ya takwimu.
Hakuna foleni mpya na/au makundi yatakayotengenezwa baada ya usanikishaji wa moduli ya takwimu.
Usanidi chaguo-msingi wa moduli ya usajili inawapa mawakala wote wenye ruhusa za kundi "takwimu" ufikivu kwenye moduli ya takwimu.
Ufikivu kuendana na mipangilio ya ruhusa:
soma andika. Inaruhusu kusanidi takwimu na ripoti.
soma tu. Inaruhusu kuzalisha ripoti na takwimu zilizosanidiwa tayari.
Msimamizi wa OTRS anaamua kama mawakala wenye haki za kuzalisha ripoti zilizosanidiwa kabla wanapewa haki za kusoma tu kwenye kundi la "takwimu", au kama makundi yao husika yanaongezwa katika moduli ya usajili kwenye SysCondig.
Makundi ya SysConfigKiunzi:Kiini::Takwimu, Kiunzi:Kiini::Takwimu::Grafu na Kiunzi:Mazingirayambele::Wakala::Takwimu ina usanidi wote wa parameta kwa ajili ya mpangilio wa msingi wa moduli ya takwimu. Zaidi, parameta ya usanidi $Self->{'Frontend::Module'}->{'AgentStats'} inadhibiti mpangilio na usajili wa moduli na ikoni ndani ya moduli ya takwimu.
Kwa ujumla, hakuna msimamizi wa mfumo anayehitajika kwa operesheni, usanidi na matengenezo ya moduli ya takwimu. Hata hivyo, taarifa kidogo za msimamizi wa mfumo zinatolewa katika pointi hii.
Njia za mafaili zinarejea kwenye mipangilio orodha midogo ya mpangilio
orodha wa nyumbani wa OTRS (kwa kesi nyingi/opt/otrs
).
Usanidi wote wa ripoti unafanyika na kusimamiwa katika XML, na hivyo kuhifadhiwa katika jedwali la hifadhidata "xml_storage". Moduli nyingine ambazo maudhui yake yanawasilishwa katika muundo huu wa xml zinatumia hili jedwali pia.
Mafaili yafuatayo ni muhimu kwa moduli ya takwimu kufanya kazi vizuri:
Kernel/System/Stats.pm
Kernel/Modules/AgentStats.pm
Kernel/System/CSV.pm
Kernel/Output/HTML/Standard/AgentStatsOverview.dtl
Kernel/Output/HTML/Standard/AgentStatsDelete.dtl
Kernel/Output/HTML/Standard/AgentStatsEditSpecification.dtl
Kernel/Output/HTML/Standard/AgentStatsEditRestrictions.dtl
Kernel/Output/HTML/Standard/AgentStatsEditXaxis.dtl
Kernel/Output/HTML/Standard/AgentStatsEditValueSeries.dtl
Kernel/Output/HTML/Standard/AgentStatsImport.dtl
Kernel/Output/HTML/Standard/AgentStatsPrint.dtl
Kernel/Output/HTML/Standard/AgentStatsView.dtl
Kernel/System/Stats/Dynamic/Ticket.pm
bin/otrs.GenerateStats.pl
Kama matokeo ya takwimu yatawekwa kwenye hifadhi muda au la inaweza kusetiwa
kwenye usanidi. Matokeo ya ripoti ya kwenye hifadhi muda yanahifadhiwa kama
mafaili kwenye mpangilio orodha var/tmp
wa usakinishaji
wa OTRS (kwa mara nyingi /opt/otrs/var/tmp
).
Takwimu za hifadhi muda zinaweza kujulikana kwa kiambishi awali "Takwimu".
Kama data zimepotea, hakuna madhara makubwa yaliyosababishwa. Mara nyingine ripoti itakapoitwa, moduli ya hali haitatafuta faili hilo tena na kwa hiyo itazalisha ripoti mpya. Bila shaka hii itachukua muda zaidi kidogo kufanyika.
Hili faili linahifadhiwa kwenye mpangilio orodha
bin
. Inawezesha uzalishaji wa ripoti katika tungo amri.
Kama mfano, ona ita ya tungo amri katika hati ifuatayo.
bin> perl otrs.GenerateStats.pl -n 10004 -o /output/dir
Hati: Kuzalisha ripoti kutoka kwenye tungo amri.
Ripoti kutoka kwenye usanidi wa takwimu "Stat#10004" unazalishwa na
kuhifadhiwa kama csv katika mpangilio orodha
/output/dir
.
Ripoti iliyotengenezwa pia inaweza kutumwa kama barua pepe. Taarifa zaidi zinaweza patikana kwa agizo katika hati chini.
bin> perl otrs.GenerateStats.pl --help
Hati: Kupata taarifa kuhusu faili la otrs.GenerateStats.pl.
Kwa kawaida haina maana kutengeneza ripoti kwa mikono kupitia tungo amri, kwani moduli ya takwimu ina kiolesura michoro rahisi. Lakini, kutengeneza ripoti kwa mikono inaleta maana ikiunganishwa na kazi za mfumo zilizopangwa.
Fikiria mazingira yafuatayo: Kila siku ya kwanza ya mwezi, wakuu wa idara wanataka kupokea ripoti ya mwezi uliopita. Kwa kujumuisha kazi za mfumo zilizopangwa na muito wa tungo amri ripoti zinaweza kutumwa kwa kiotomatiki kwa barua pepe.
Moduli ya takwimu inawezesha uzalishaji wa takwimu tuli. Kwa kila takwimu tuli faili linakuwepo ambalo maudhui yake yamefafanuliwa kwa ufasaha.
Njia hii, takwimu changamano zinaweza kuzalishwa. Kasoro yake ni hazibadiliki kirahisi.
Mafili yanahifadhiwa kwenye mpangilio orodha
Kernel/System/Stats/Static/
.
Kabla ya OTRS 1.3 na 2.0 uzalishaji wa ripoti / takwimu ulishawezeshwa. Ripoti tofauti za matoleo ya OTRS 1.3 na 2.0 ambazo ziliundwa kufikia mahitaji ya wateja zinaweza kutumika katika matoleo ya OTRS ya sasa pia.
Mafaili lazima yahamishwe kutoka njia
Kernel/System/Stats/
kwenda
Kernel/System/Stats/Static/
. Pia jina la kifurushi cha
hati hiyo lazima kirekebishwe na "::Tuli"
Mfano ufwatao unaonyesha jinsi njia ya kwanza inavyofanyiwa marekebisho.
package Kernel::System::Stats::AccountedTime;
package Kernel::System::Stats::Static::AccountedTime;
"Sio muhimu wakati wote kuunda vitu ambavyo vipo tayari..... "
Moduli ya takwimu inatoa ripoti chaguo-msingi mbali mbali. Ripoti ambazo ni
za muhimu kwa watumiaji wote wa OTRS baadaye zitaongezwa kwenye seti ya
ripoti chaguo-msingi za kifurushi cha moduli za takwimu. Ripoti
chaguo-msingi zinahifadhiwa katika muundo wa xml wa moduli za takwimu kwenye
mpangilio orodha scripts/test/sample/
.