Sehemu zinazobadilika

Utangulizi
Usanidi
Kuongeza Sehemu Inayobadilika
Nakala ya Usanidi wa Sehemu Inayobadilika
Usanidi wa Eneo la nakala ya Sehemu Zinazobadilika
Usanidi wa Sehemu Inayobadilika ya Kisanduku tiki
Usanidi wa Kikunjuzi cha Sehemu Inayobadilika
Uteuzi Anuwai wa Usanidi wa Sehemu Inayobadilika
Usanidi wa Sehemu Inayobadilika ya Tarehe
Usanidi wa Tarehe / Muda wa Sehemu Inayobadilika
Kuhariri sehemu inayobadilika
Kuonyesha Sehemu Inayobadilika kwenye Skrini
Onyesha Mifano
Kuweka Thamani Chaguo-msingi kwa kutumia Moduli ya Tukio la Tiketi
Seti thamani ya chaguo-msingi kwa Upendeleo wa mtumiaji

Utangulizi

Sehemu inayobadilika ni sehemu ya aina maalumu katika OTRS, iliyotengenezwa kupanua taarifa iliyohifadhiwa katika makala au tiketi. Hizi makala si funge kwenye mfumo na zinaweza kutokea kwenye skrini maalumu tu, zinaweza kuwa za lazima au si za lazima, na uwasilishwaji wake kwenye skrini unategemeana na aina ya sehemu iliyofafanuliwa wakati wa utengenezaji wake kulingana na data inayoshikiliwa na sehemu. Kwa mfano, kuna sehemu za kushikilia nakala, tarehe, chaguo la vitu, na kadh.

Sehemu zinazobadilika ni mageuko ya spishi ya sehemu TiketiHuruNakala TiketiHuruFunguo TiketiHuruMuda, MakalaHuruNakala na MakalaHuruFunguo ambazo zilkuwa zikitumiwa sana katika OTRS 3.0 na kabla. Kikomo cha hizi "Sehemu Huru" ilikuwa ni zinaweza kufafanuliwa mpaka sehemu 16 (nakala au kunjuzi) na sehemu 6 za muda kwa ajili ya tiketi na sehemu 3 (nakala au kunjuzi) kwa kila nakala tu, sio zaidi.

Sasa kwa kutumia sehemu zinazobadilika kikomo katika nambari ya sehemu kwa tiketi au makala kimeondolewa, unaweza kutengeneza sehemu nyingi zinazobadilika unazotaka aidha kwa tiketi au makala. Na zaidi ya hapo, kiunzi nyuma ya sehemu zinazobadilika kinaandaliwa kushughulikia sehemu zilizogeuzwa kukufaa kwa ajili ya vitu vingine kuachana na tiketi na makala tu.

Kiunzi hiki ambacho kinashughulikia sehemu zinazobadilika kimetengenezwa kwa kutumia mbinu ya moduli, ambapo kila aina ya sehemu inayobadilika inaweza kuonekana kama moduli ya programu-jalizi kwa ajili ya kiunzi. Hii inamaanisha aina mbali mbali ya sehemu zinazobadilika zinaweza kupanuliwa kirahisi kwa kutumia moduli za umma za OTRS, vifaa vya nyongeza vya vipengele vya OTRS, maendeleo yaliyogeuzwa kukufaa ya OTRS, na maendeleo mengine yaliyogeuzwa kukufaa.

Aina zifuatazo za sehemu zinazobadilika zimejumuishwa kwenye toleo hili:

  • Nakala (nakala ya mstari mmoja)

  • Eneo la nakala (nakala za mistari mingi)

  • Kisanduku tiki

  • Kunjuzi (chaguo moja, thamani nyingi)

  • Uchaguzi anuwai (uchaguzi nyingi, thamani nyingi)

  • Tarehe

  • Tarehe / Muda

Usanidi

By default, a clean installation of OTRS comes with two pre-installed internal dynamic fields, which cannot be removed. If you plan to use such fields in tickets or articles you need to create new, custom dynamic fields.

Usanidi wa sehemu zinazobadilika umegawanyika katika nyanja mbili, kuongeza sehemu mpya inayobadilika au kusimamia iliyopo unahitaji kwenda paneli ya "Msimamizi" kwenye kiungo "Sehemu Zinazobadilika". Kuonyesha, kuonyesha kwa ulazima au kuficha sehemu inayobadilika katika skrini moja unahitaji kubadilisha mipangilio ya OTRS katika skrini ya "SysConfig".

Kuongeza Sehemu Inayobadilika

Bofya kwenye kitufe cha "Msimamizi" kilicho kwenye mwambaa wa uabiri, kisha bofya kwenye kiungo "Sehemu Inayobadilika" ndani ya boksi la "Mipangilio ya Tiketi" lililo ndani kushoto mwa skrini. Mapitio ya sehemu zinazobadilika itaonekana kama ifuatavyo:

Figure: Dynamic fields overview screen.

Tambua kwamba hii skrini itabadilika kadri uongezavyo sehemu zinazobadilka kuorodhesha sehemu zote zinazobadilika. Hii skrini inaweza tayari kuwa na baadhi ya sehemu kama usanikishaji ulirekebishwa kutoka toleo la zamani la OTRS.

Vitendo kwenye ufito wa pembeni kushoto kwa skrini vinaelezea uwezekano wa aina mbili: Makala na Tiketi, kila moja ina uchaguzi kunjuzi wa sehemu zinazobadilika.

Note

Usanikishaji wa kifurushi cha OTRS unaweza kuongeza vitu katika ufito wa pembeni.

Utaratibu wa kawaida wa kutengenza sehemu zinazobadilika ni:

  • Bofya kwenye kitu cha sehemu inayobadilika unachotaka kwenye mwambaa upande wa Kitendo.

  • Bofya kwenye aina ya sehemu inayobadilika unayotaka kuongeza kutoka kwenye orodha.

  • Jaza usanidi

  • Hifadhi

Maongezi ya usanidi wa sehemu zinazobadilika yamegawanywa katika sehemu mbili, upande wa juu ni wa kawaida baina ya sehemu zote na upande wa chini unaweza kuwa tofauti kwa aina moja ya sehemu inayobadilika kwenda nyingine.

Mipangilio ya ujumla ya sehemu zinazobadilika:

  • Jina: Lazima, kipekee, herufi na nambari tu zinaruhusiwa,

    Hili ni jina la ndani la sehemu, linatumika kwa mfano kuonyesha au kuficha sehemu katika skrini. Mabadiliko yoyote ya jina la sehemu (haishauriwi) inahitaji usasishaji kwa mikono wa mipangilio ya "SysConfig" ambapo sehemu ina rejea.

  • Lebo: Lazima

    Hili ndio jina la sehemu litakaloonyeshwa kwenye skrini, ina msaada kwa tafsiri.

    Note

    Tafsiri za lebo inabidi ziongezwe kwa mikono kwenye mafaili ya utafsiri wa lugha.

  • Oda ya sehemu: Lazima.

    Inafafanua oda tegemezi ambayo sehemu itaonyeshwa kwenye skrini, kwa chaguo-msingi kila sehemu mpya ina sehemu ya mwisho, mabadiliko katika huu mpangilio utaathiri oda ya sehemu nyingine zinazobadilika zilizotengenezwa.

  • Uhalali: Lazima.

    Sehemu inayobadilika batili haitaonyeshwa katika skrini yoyote, hata kama imesanidiwa kuonyeshwa.

  • Aina ya sehemu: Lazima, Soma tu.

    Inaonyesha aina ya sehemu iliyochaguliwa.

  • Aina ya kitu: Lazima, Soma tu.

    Inaonyesha upeo wa sehemu.

Note

Kuonyesha mipangilio ya kila aina maalumu ya sehemu sehemu chache zitaongezwa kwenye mfano wetu. Hizi sehemu mpya zitafanyiwa marejeo kwenye vifungu vya mbele.

Kwa mfano ufwatao sehemu zote zinazobadilika zitatengenezwa kwa ajili ya kitu cha Tiketi kama unahitaji kutengeneza sehemu inayobadilika kwa kitu cha Makala, chagua tu sehemu kutoka kwenye orodha kunjuzi ya Makala.

Table 4.6. Sehemu zifuatazo zitaongezwa kwenye mfumo:

Jina Lebo Aina
Sehemu1 Sehemu yangu 1 Nakala
Sehemu2 Sehemu yangu 2 Eneo la nakala
Sehemu3 Sehemu yangu 3 Kisanduku tiki
Sehemu4 Sehemu yangu 4 Kunjuzi
Sehemu5 Sehemu yangu 5 Chaguanyingi
Sehemu6 Sehemu yangu 5 Tarehe
Sehemu7 Sehemu yangu 6 Tarehe / Muda

Nakala ya Usanidi wa Sehemu Inayobadilika

Sehemu inayobadilika ya Nakala inatumika kuhifadhi tungo ya mstari mmoja.

Nakala ya mpangilio wa sehemu inayobadilika:

  • Thamani ya chaguo-msingi: Hiari.

    Hii ni thamani ya kuonyeshwa kwa kawaida kwenye shrini za kuhariri (kama Simu Npya ya Tiketi au Tunga Tiketi)

  • Onyesha kiungo: Hiari.

    Kama imeseetiwa, thamani ya sehemu itabadilishwa kuwa kiungo kinachobonyezeka kwa ajili ya skrini za kuonyesha (kama kuza tiketi au mapitio).

    Kwa mfano, kama "Onyesha kiungo" imesetiwa kuwa "http://www.otrs.com", kubofya kwenye thamani ya sehemu kitafanya kivinjari chako kufungua ukurasa wa tovuti wa OTRS.

    Note

    The use of [% Data.NameX | uri %] in the Set link value, where NameX is the name of the field will add the field value as part of the link reference.

Kielelezo: Maongezi ya usanidi wa Nakala ya Sehemu inayobadilika..

Usanidi wa Eneo la nakala ya Sehemu Zinazobadilika

Eneo la nakala ya sehemu zinazobadilika hutumika kuhifadhi tungo za mstari zaidi ya mmoja

Mpangiio wa sehemu zinazobadilika za eneo la nakala

  • Idadi ya safu: Hiari, namba kamili.

    Inatumika kufafanua urefu wa sehemu kwenye skrini za kuhariri (kama Simu Mpya ya Tiketi au Tunga Tiketi).

  • Idadi ya safu: Hiari, namba kamili.

    Hii thamani inatumika kufafanua upana wa sehemu kwenye skrini za kuhariri.

  • Thamani ya chaguo-msingi: Hiari.

    Hii ni thamani itakayo onyeshwa kwa kawaida kwenye skrini za kuhariri (inaweza kuwa nakala ya zaidi ya mstari mmoja).

Kielelezo: Maongezi ya usanidi wa Nakalaeneo ya Sehemu inayobadilika..

Usanidi wa Sehemu Inayobadilika ya Kisanduku tiki

Sehemu inayobadilika ya kisanduku tiki inatumika kuhifadhi thamani ya kweli au uongo, inayowakilishwa na boksi lenye tiki au lisilo na tiki.

Mipangilio ya sehemu inayobadilika ya kisanduku tiki:

  • Thama ya Kawaida: Lazima.

    Hii ndiyo thamani ya kuonyeshwa kwa chaguo-msingi katika skrini za kuhariri (kama Tiketi Mpya ya Simu au Unda Tiketi), thamani chaguo-msingi la hii sehemu ni uchaguzi uliofungwa ambao unaweza kutikiwa au kutotikiwa.

Kielelezo: Usanidi wa maongezi wa sehemu inayobadilika ya kisanduku tiki.

Usanidi wa Kikunjuzi cha Sehemu Inayobadilika

Kikunjuzi cha sehemu inayobadilika kinatumika kuhifadhi thamani moja, kutoka kwenye orodha iliyofungwa.

Mipangilio ya sehemu kunjuzi inayobadilika:

  • Thamani zinazowezekana: Lazima.

    Orodha ya thamani za kuchagua. Kama ikitumika, thamani mpya ni muhimu kubainisha Ufunguo (thamani ya ndani) na Thamani (thamani ya kuonyeshwa).

  • Thamani ya chaguo-msingi: Hiari.

    Hii ndiyo thamani ya kuonyeshwa kwa chaguo-msingi katika skrini za kuhariri (kama Tiketi Mpya ya Simu au Unda Tiketi), thamani chaguo-msingi la hii sehemu ni uchaguzi uliofungwa unaofafanuliwa na thamani Ziwezekanazo.

  • Ongeza sehemu tupu: Lazima, (Ndio/Hapana).

    Kama hili chaguo limeamilishwa thamani ya ziada inafafanuliwa kuonyesha "-" kwenye orodha ya thmani ziwezekanazo, hii thamani maalumu ni wazi ndani.

  • Tafsiri thamani: Lazima, (Ndio/Hapana).

    Huu mpangilio unatumika kuweka alama thamani zinazoweza kutafsiriwa za hii sehemu. Thamani zinazoonyeshwa tu ndio zita tafsiriwa, thamani za ndani hazita athiriwa, utafsiri wa thamani inabidi uongezwe kwa mikono kwenye mafaili ya lugha.

  • Onyesha kiungo: Hiari.

    Kama imesetiwa, thamani ya sehemu itabadilishwa kuwa kiungo cha HTP kinachobonyezeka kwa ajili ya skrini za kuonyesha (kama Kuza au mapitio).

    Kwa mfano, kama Onyesha kiungo imesetiwa kuwa "http://www.otrs.com", kubofya kwenye thamani hii ya sehemu kutafanya kivinjari chako kufumgua ukurasa wa tovuti wa OTRS.

    Note

    The use of [% Data.NameX | uri %] in the Set link value, where NameX is the name of the field, will add the field value as part of the link reference.

Kielelezo: Maongezi ya usanidi wa Kikunjuzi cha Sehemu inayobadilika.

Uteuzi Anuwai wa Usanidi wa Sehemu Inayobadilika

Uteuzi Anuwai wa sehemu inayobadilika unatumika kuhifadhi thamani anuai, kutoka kwenye orodha iliyofungwa.

Mipangilio ya sehemu inayobadilika ya uteuzi anuwai:

  • Thamani zinazowezekana: Lazima.

    Orodha ya thamani za kuchagua. Wakati wa kuongeza vifaa vya nyongeza kwenye orodha, ni muhimu kubainisha Ufunguo (thamani ya ndani) na Thamani (thamani ya kuonyeshwa).

  • Thamani ya chaguo-msingi: Hiari.

    Hii ndiyo thamani ya kuonyeshwa kwa chaguo-msingi katika skrini za kuhariri (kama Tiketi Mpya ya Simu au Unda Tiketi), thamani chaguo-msingi la hii sehemu ni uchaguzi uliofungwa kama ulivyofafanuliwa na thamani Ziwezekanazo.

  • Ongeza sehemu tupu: Lazima, (Ndio/Hapana).

    Kama hili chaguo limeamilishwa thamani ya ziada inafafanuliwa kuonyesha "-" katika orodha ya thamani ziwezekanazo. Hii thamani maalumu ni tupu ndani

  • Tafsiri thamani: Lazima, (Ndio/Hapana).

    Huu mpangilio unatumika kuweka alama thamani zinazoweza kutafsiriwa za hii sehemu. Thamani zinazoonyeshwa tu ndio zita tafsiriwa, thamani za ndani hazita athiriwa, utafsiri wa thamani inabidi uongezwe kwa mikono kwenye mafaili ya lugha.

Kielelezo: Maongezi ya usanidi wa Uteuzi Anuwai wa Sehemu inayobadilika.

Usanidi wa Sehemu Inayobadilika ya Tarehe

Sehemu inayobadilika ya Tarehe inatumika kuhifadhi thamani ya tarehe (Siku, Mwezi na Mwaka).

Mipangilio ya sehemu inayobadilika ya tarehe:

  • Chaguo-msingi la utofauti wa tarehe: Hiari, Namba kamili.

    Idadi ya sekunde (hasi au chanya) kati ya tarehe ya sasa na tarehe iliyochaguliwa kuonyeshwa kwa chaguo-msingi katika skrini za kuhariri (kama Tiketi Mpya Simu au Unda Tiketi).

  • Fananua kipindi cha miaka: Lazima (Ndio / Hapana).

    Inatumika kufafanua idadi maalumu ya miaka ya nyuma na baadaye kwa kutegemeana na tarehe ya sasa ya mwaka uliochaguliwa kwa hii sehemu, kama imesetiwa kuwa Ndiyo machaguo yafwatayo yanapatikana:

    • Miaka ya nyuma: Hiari, Namba kamili chanya.

      Fafanua idadi ya miaka ya nyuma kutoka siku ya sasa kuonyesha chaguo la mwaka kwa hii sehemu inayobadilika katika skrini za kuhariri.

    • Miaka ya mbeleni: Hiari, Namba kamili chanya.

      Fafanua idadi ya miaka ya mbeleni kutoka siku ya sasa kuonyesha katika chaguo la mwaka kwa hii sehemu inayobadilika katika skrini za kuhariri.

  • Onyesha kiungo: Hiari.

    Kama imesetiwa, thamani ya sehemu itabadilishwa kuwa kiungo cha HTP kinachobonyezeka kwa ajili ya skrini za kuonyesha (kama Kuza au mapitio).

    Kwa mfano, kama Onyesha kiungo imesetiwa kuwa "http://www.otrs.com", kubofya kwenye thamani hii ya sehemu kutafanya kivinjari chako kufumgua ukurasa wa tovuti wa OTRS.

    Note

    The use of [% Data.NameX | uri %] in the Set link value, where NameX is the name of the field will add the field value as part of the link reference.

Kielelezo: Maongezi ya usanidi wa Tarehe ya Sehemu inayobadilika.

Usanidi wa Tarehe / Muda wa Sehemu Inayobadilika

Sehemu inayobadilika ya Tarehe / Muda inatumika kuhifadhi thamani ya ttarehe muda (Dakika, Masaa. Siku, Mwezi na Mwaka).

Mipangilio ya sehemu inayobadilika ya tarehe / muda:

  • Chaguo-msingi la utofauti wa tarehe: Hiari, Namba kamili.

    Idadi ya sekunde (hasi au chanya) kati ya tarehe ya sasa na tarehe iliyochaguliwa kuonyeshwa kwa chaguo-msingi katika skrini za kuhariri (kama Tiketi Mpya Simu au Unda Tiketi).

  • Fananua kipindi cha miaka: Lazima (Ndio / Hapana).

    Inatumika kuseti nambari ya miaka iliyofafanuliwa huko nyuma na mbeleni kutoka kwenye tarehe ya sasa katika chaguo la mwaka la sehemu hii, kama imesetiwa kuwa Ndiyo machaguo yafwatayo yanapatikana:

    • Miaka ya nyuma: Hiari, Namba kamili chanya.

      Fafanua idadi ya miaka ya nyuma kutoka siku ya sasa kuonyesha chaguo la mwaka kwa hii sehemu inayobadilika katika skrini za kuhariri.

    • Miaka ya mbeleni: Hiari, Namba kamili chanya.

      Fafanua idadi ya miaka ya mbeleni kutoka siku ya sasa kuonyesha katika chaguo la mwaka kwa hii sehemu inayobadilika katika skrini za kuhariri.

  • Onyesha kiungo: Hiari.

    Kama imesetiwa, thamani ya sehemu itabadilishwa kuwa kiungo cha HTP kinachobonyezeka kwa ajili ya skrini za kuonyesha (kama Kuza au mapitio).

    Kwa mfano, kama Onyesha kiungo imesetiwa kuwa "http://www.otrs.com", kubofya kwenye thamani hii ya sehemu kutafanya kivinjari chako kufumgua ukurasa wa tovuti wa OTRS.

    Note

    The use of [% Data.NameX | uri %] in the Set link value, where NameX is the name of the field will add the field value as part of the link reference.

Kielelezo: Maongezi ya usanidi wa Tarehe / Muda wa Sehemu inayobadilika.

Kuhariri sehemu inayobadilika

Skrini ya mapitio ya sehemu inayobadilika iliyojazwa (na mifano iliyopita) inatakiwa ionekane kama:

Kielelezo: Skrini ya mapitio ya sehemu zinazobadilika iliyojazwa na data za sampuli.

Kubadilisha au kuhariri sehemu inayobadilika lazima uwe na sehemu moja iliyofafanuliwa, chagua sehemu ambayo tayari imejazwa kutoka kwenye skrini ya mapitio ya sehemu zinazobadilika na sahihisha mipangilio.

Note

Sio sehemu zote zinazobadilika zinaweza kubadilishwa, aina ya Sehemu na aina ya Kitu zimefungwa kutoka kwenye machaguo ya sehemu na haziwezi kubadilishwa.

Haishauriwi kubadilisha jina la ndani la sehemu, lakini lebo inaweza kubadilishwa mda wowote. Kama jina la ndani limebadilishwa mipangilio yote ya "SysConfig" ambayo ina marejeo kwenye sehemu hiyo yanahitaji kusasishwa na pia mapendeleo ya mtumiaji (kama imefafanuliwa).

Kuonyesha Sehemu Inayobadilika kwenye Skrini

Kuonyesha sehemu inayobadilika kwenye skrini fulani kuna masharti mawili ya lazima:

  1. Sehemu inayobadilika lazima iwe halali.

  2. Sehemu inayobadilika lazima isetiwe kuwa 1 au 2 kwenye skrini ya usanidi.

Fuata hatua hizi kuonyesha sehemu inayobadilika katika skrini

  • Kuwa na uhakika kwamba sehemu inayobadilika imesetiwa kuwa halali, unaweza kuona uhalali wa sehemu kutoka kwenye skrini ya mapitio ya sehemu inayobadilika. Seti kuwa halali kwa kuhariri sehemu kama ikihitajika.

  • Fungua "sysconfig" na chagua "Tiketi" kutoka kwenye orodha kunjuzi katika mwambaa upande wa Vitendo ulio katika upande wa kushoto wa skrini.

    Note

    Pia unaweza kutafuta "SehemuInayobadilika" katika kisanduku cha kutafuta juu au ufunguo wa "sysconfig" moja kwa moja kama unaujua.

  • Tambua mpangilio kundi dogo kwa skrini unayoitafuta na kibonyeze. Kwa mfano "Mazingira ya mbele::Wakala::Tiketi::OnaSimuMpya".

  • Tafuta mpangilio uanoishia na "###SehemuInayobadilika". Kwa mfano "Tiketi::Mazingira ya mbele::WakalaTiketiSimu###SehemuInayobadilika".

  • Kama mpangilio uko tupu au hauna jina linalotakiwa la sehemu inayobadilika, bofya kwenye kitufe "+" kuongeza ingizo jipya. Kwa mfano Ufunguo: Sehemu1, Maudhui: 1.

    Kama mpangilio tayari una orodha ya jina la sehemu inayobadilika kuwa na uhakika kwamba imesetiwa kuwa "1" ili kuonyesha hiyo sehemu au kuwa "2" kuonyesha kwa ulazima.

  • Hifadhi usanidi kwa kubofya katika kitufe cha "Sasisha" na chini ya skrini na abiri kwenda kwenye skrini ambayo unataka sehemu ionyeshwe.

Onyesha Mifano

Ifuatayo ni mifano ya usanidi wa "sysconfig" kuonyesha au kuficha sehemu zinazobadilika katika skrini tofauti.

Example 4.21. Amilisha Sehemu1 katika Simu Mpya Tiketi Skrini.

  • Umbo: Kundi. Tiketi

  • Kundi-dogo: Mazingira ya mbele::Wakala::Tiketi::OnaSimuMpya

  • Mpangilio: Tiketi::Mazingira ya mbele::WakalaTiketiSimu###SehemuInayobadilika

  • Thamani:

    Ufunguo Maudhui
    Sehemu1 1

Kielelezo: Sehemu1 katika Simu Mpya Tiketi Skrini.


Example 4.22. Amilisha Sehemu1 katika Simu Mpya Tiketi Skrini kwa ulazima.

  • Umbo: Kundi. Tiketi

  • Kundi-dogo: Mazingira ya mbele::Wakala::Tiketi::OnaSimuMpya

  • Mpangilio: Tiketi::Mazingira ya mbele::WakalaTiketiSimu###SehemuInayobadilika

  • Thamani:

    Ufunguo Maudhui
    Sehemu1 2

Kielelezo: Sehemu1 katika Simu Mpya Tiketi Skrini kwa ulazima.


Example 4.23. Amilisha sehemu mbali mbali katika Simu Mpya Tiketi Skrini.

  • Umbo: Kundi. Tiketi

  • Kundi-dogo: Mazingira ya mbele::Wakala::Tiketi::OnaSimuMpya

  • Mpangilio: Tiketi::Mazingira ya mbele::WakalaTiketiSimu###SehemuInayobadilika

  • Thamani:

    Ufunguo Maudhui
    Sehemu1 1
    Sehemu2 1
    Sehemu3 1
    Sehemu4 1
    Sehemu5 1
    Sehemu6 1
    Sehemu7 1

Kielelezo: Sehemu mbali mbali katika Simu Mpya Tiketi Skrini kwa ulazima.


Example 4.24. Lemaza baadhi ya sehemu katika Simu Mpya Tiketi Skrini.

  • Umbo: Kundi. Tiketi

  • Kundi-dogo: Mazingira ya mbele::Wakala::Tiketi::OnaSimuMpya

  • Mpangilio: Tiketi::Mazingira ya mbele::WakalaTiketiSimu###SehemuInayobadilika

  • Thamani:

    Ufunguo Maudhui
    Sehemu1 1
    Sehemu2 0
    Sehemu3 1
    Sehemu4 0
    Sehemu5 1
    Sehemu6 0
    Sehemu7 1

Kielelezo: Baadhi ya sehemu zilizolemazwa katika Simu Mpya Tiketi Skrini kwa ulazima.


Example 4.25. Amilisha Sehemu1 katika Skrini Kuza Tiketi.

  • Umbo: Kundi. Tiketi

  • Kundi-dogo: Mazingira ya mbele::Wakala::Tiketi::OnaKuza

  • Mpangilio: Tiketi::Mazingira ya mbele::WakalaTiketiKuza###SehemuInayobadilika

  • Thamani:

    Ufunguo Maudhui
    Sehemu1 1

Kielelezo: Sehemu1 katika Skrini Kuza Tiketi.


Example 4.26. Amilisha Sehemu1 katika Mapitio ya Skrini Ndogo za Tiketi.

  • Umbo: Kundi. Tiketi

  • Kudni-dogo: Mazingira ya mbele::Wakala::TiketiMapitio

  • Mpangilio: Tiketi::Mazingira ya mbele::MapitioMadogo###SehemuInayobadilika

  • Thamani:

    Ufunguo Maudhui
    Sehemu1 1

Kielelezo: Sehemu1 katika Mapitio ya Skrini Ndogo za Tiketi.

This setting affects: Escalation View, Locked View, Queue View, Responsible View, Status View, Service View and Watch View screens.


Kuweka Thamani Chaguo-msingi kwa kutumia Moduli ya Tukio la Tiketi

Tukio la tiketi (mf. TengenezaTiketi) linaweza kuchochea thamani kusetiwa kwa sehemu fulani, kama sehemu bado haina thamani.

Note

Kwa kutumia njia hii thamani chaguo-msingi, haionekani katika skrini za kuhariri (mf. Simu Mpya Tiketi) kwa kuwa thamani imesetiwa baada ya utengenezaji wa tiketi.

Kuamilisha hiki kipengele ni muhimu kuwezesha mpangilio ufwatao: "Tiketi::TukioModuliTuma###TiketiSehemuInayobadilikaChaguo-msingi".

Example 4.27. Amilisha Sehemu1 katika kitendo cha TengenezaTiketi.

  • Umbo: Kundi. Tiketi

  • Kundi-dogo: Kiini::TiketiSehemuInayobadilikaChaguo-msingi

  • Mpangilio: Tiketi::TiketiSehemuInayobadilikaChaguo-msingi###Elementi1

    Note

    Huu usanidi unaweza kusetiwa katika moja ya tiketi 16::TiketiSehemuInayobadilikaChaguo-msingi###Mipangilio ya elementi.

    Kama zaidi ya sehemu 16 zinahitajika kuaanzishwa faili la XML klililogeuzwa kukufaa lazima liwekwe kwenye mpangilio orodha $OTRS_HOME/Kernel/Config/files kuendeleza kipengele hiki.

  • Thamani:

    Ufunguo Maudhui
    Kitendo TengenezaTiketi
    Jina Sehemu1
    Thamani thamani mpya


Seti thamani ya chaguo-msingi kwa Upendeleo wa mtumiaji

Chaguo-msingi la sehemu inayobadilika inaweza kubadilishwa na thamani ziliyofafanuliwa na mtumiaji zilizohifadhiwa kwenye mapendeleo ya mtumiaji.

Kutumia njia hii, thamani ya chaguo-msingi la hiyo sehemu litaonyeshwa kwenye skrini yoyote ambapo sehemu hiyo imeamilishwa (kama sehemu tayari haina thaamani nyingine).

Mipangilio ya "sysconfig" ya "MapendeleoMakundi###SehemuInayobadilika" inayopatikana katika Kundi dogo la "Mazingira ya mbele::Wakala::Mapendeleo". Huu mpangilio ni mfano wa jinsi ya kutengeneza ingizo katika skrini ya Mapendeleo ya Mtumiaji kuseti thamani ya chaguo-msingi la sehemu inayobadilika pweke kwa ajili ya mtumiaji aliyechaguliwa. Kiwango cha juu cha huu mpangilio ni inaruhusu matumizi ya sehemu moja tu inayobadilika. Kama sehemu mbili au zaidi zitatumia hiki kipengele, ni muhimu kutengeneza usanidi wa faili la XML uliogeuzwa kukufaa kuongeza mipangilio zaidi inayofanana na huu.

Note

Kumbuka, kama mipangilio zaidi imeongezwa katika XML mpya kila jina la mpangilio linahitaji kuwa la kipekee kwenye mfumo na tofauti na "MapendeleoMakundi###SehemuInayobadilika". kwa mfano: MapendeleoMakundi###101-SehemuInayobadilika-Sehemu1, MapendeleoMakundi###102-SehemuInayobadilika-Sehemu2, MapendeleoMakundi###Sehemu-yangu1, MapendeleoMakundi###Sehemu-yangu2, na kadh.

Example 4.28. Amilisha Sehemu1 katika mapendeleo ya Mtumiaji.

  • Umbo: Kundi. Tiketi

  • Kundi-dogo: Mazingira ya mbele::Wakala::Mapendeleo

  • Mpangilio: MakundiMapendeleo###101-SehemuInayobadilika-Sehemu1

  • Thamani:

    Ufunguo Maudhui
    Kitendo TengenezaTiketi
    Amilifu 1
    fungu Ingizo
    Safuwima Mipangilio mingine
    Data: [% Env("UserDynamicField_Field1") %]
    Ufunguo: Sehemu yangu 1
    Lebo: Chaguo-msingi kwa: Sehemu yangu 1
    Moduli: Kiini::Matokeo::HTML::MapendeleoUjumla
    MapendeleoUfunguo: MtumiajiSehemuInayobadilika_Sehemu1
    Kipaumbele: 7000

Kielelezo: Sehemu1 katika Skrini ya mapendeleo ya mtumiaji.