Kuingia kwa mara ya kwanza

Fikia kwenye skrini ya kuingia kama ilivyoelezewa katika kifungu Kiolesura cha tovuti cha wakala. Ingiza jina ka mtumiaji na nywila. Kwa kuwa mfumo ndio kwanza umesakinishwa na hakuna mtumiaji aliyetengenezwa, ingia kama msimamizi wa OTRS kwanza, kwa kutumia 'root@localhost' kama jina la mtumiaji na 'root' kama nywila.

Warning

Hii data ya akaunti ni halali kwa kila usakinishaji mpya wa mfumo wa OTRS. Unatakiwa kubadilisha nywila ya msimamizi wa OTRS mapema iwezekanavyo! Hii inaweza kufanyika kupitia skrini ya mapendeleo kwa ajili ya akaunti ya msimamizi wa OTRS.

Kama hutaki kuingia kama msimamizi wa OTRS, ingiza jina la mtumiaji na nywila za akaunti yako ya kawaida ya wakala.

Ikitokea umesahau nywila yako, unaweza kuuomba mfumo nywila mpya. Bonyeza kirahisi kiungo chini ya kitufe cha kuingia, ingiza anuani yako ya barua pepe iliyosajiliwa kwenye akaunti yako ya OTRS kwenye sehemu ya maingizo, na kisha bonyeza kitufe cha kuwasilisha. (ona Kielelezo).

Kielelezo: Omba nywila mpya