Kwa nyongeza kwenye violesura vya wavuti kwa ajili ya mawakala na wateja. OTRS pia ina kiolesura cha umma ambacho kinapatikana kupitia moduli ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara. Hii moduli inahitaji kusakinishwa pekeyake. Inatoa ufikivu wa umma kwa mfumo wa maswali yanayoulizwa mara kwa mara na inaruhusu wageni kutafuta kwenye maingizo ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara bila uidhinishaji wowote maalumu.
Katika mfano wetu, kiolesura cha tovuti cha umma kinaweza kufikiwa kwa kupitia aidha ya URL zifuatazo: http://www.example.com/otrs/faq.pl , http://www.example.com/otrs/public.pl
Kielelezo: Kiolesura cha umma cha wavuti.