Kiolesura cha tovuti - mapitio

Baada ya kuingia kwa mafanikio kwenye mfumo, unakutana na kurasa ya Dashi bodi (ona Kielelezo chini). Inaonyesha tiketi zako zilizofungwa, inaruhusu ufikivu wa moja kwa moja kupitia menyu kwenda kwenye foleni, hali na muonekano wa kupanda, na pia inashikilia uchaguzi wa kutengeneza simu mpya na tiketi za barua pepe. Pia inatoa ufupisho wa haraka wa tiketi kwa kutumia vigezo tofauti.

Kielelezo: Dashibodi ya kiolesura cha wakala.

Kuboresha uwazi, kiolesura cha wavuti cha ujumla kimegawanywa katika sehemu tofauti. Safu mlalo ya juu ya kila kurasa inaonyesha baadhi ya taarifa za ujumla kama jina la mtumiaji la sasa, kitufe cha kutoka, ikoni zinazoorodhesha nambari ya tiketi zilizofungwa zenye ufikivu kamili kwao, viungo vya kutengeneza simu/tiketi za barua pepe mpya, na kadh. Pia kuna ikoni za kwenda kwenye foleni, hali, na muonekano wa upandaji.

Chini ya safu mlalo za ikoni kuna mwambaa wa uabiri. Inaonyesha menyu ambayo inakuwezesha kwenda sehemu tofauti au kuona moduli tofauti za mfumo, ikikuruhusu kutekeleza baadhi ya vitendo vya ujumla. Kubofya kwenye kitufe cha Dashibodi inakupeleka kwenye dashibodi. Kama ukibofya kwenye kitufe cha Tiketi utapata menyu ndogo yenye machaguo ya kubadilisha muonekano wa tiketi, tengeneza tiketi mpya (simu/barua pepe) au tafuta tiketi fulani. Kitufe cha Takwimu kinakupa menyu inayokuruhusu kuchagua kutoka kwenye mapitio ya takwimu zilizosajiliwa, kutengeneza mpya au kuagiza iliyopo. Kitufe cha Wateja kinakupeleka kwenye skrini ya Usimamizi wa Mteja. Kwa kubofya kitufe cha Msimamizi, unaweza kufikia moduli zote za msimamizi, ambazo zinakuruhusu kutengeneza mawakala wapya, foleni na kadh. Pia kuna kitufe cha kutafuta tiketi.

Kama programu-tumizi zozote zinazohusika zimesakinishwa pia, mf. maswali yanayoulizwa mara kwa mara au Utafiti, vitufe kufikia hizi programu-tumizi pia vinaonyeshwa.

Mwambaa mwekundu chini ya mwambaa wa uabiri unaonyesha ujumbe tofauti wa mfumo. Kama umeingia kama msimamizi wa OTRS, utapata ujumbe wa tahadhari ya kutofanya kazi kwa kutumia akaunti ya mfumo.

Chini ya kichwa cha habari cha kifungu ulichopo sasa, kuna vifungu vidogo tofauti vyenye taarifa husika kuhusu skrini unayofanya kazi, kila moja katika kisanduku tofauti.

Haya maboksi yana sehemu muhimu ya kila skrini, kwa kawaida yanaonyeshwa katika safuwima moja au tofauti, kila boksi linaweza kuhifadhi taarifa husika kuhusu skrini ya sasa kwa mfano maelekezo, ushauri, mapitio, na kadh. Pia inaonyeshwa fomu au kifaa muhimu cha kutekeleza kitendo kinachohusika kwa kila skrini, kama kwa mfano, ongeza, sasisha au futa rekodi, kagua batli, badilisha mipangilio ya mabadiliko, na kadh.

Mwisho katika upande wa chini wa ukurasa, kijachini cha tovuti kinaonyeshwa (ona Kielelezo chini). Ina viungo ili kufikia moja kwa moja tovuti rasmi ya OTRS, au kwenda upande wa juu wa kurasa.

Kwa kawaida safu mlalo ya ikoni, mwambaa wa uabiri na kijachini ziko hivyo hivyo katika skrini zote kwenye kiolesura cha tovuti.

Kielelezo: Kijachini.