Dashibodi

Dashi bodi ndiyo kurasa kuu ya mfumo, hapa unaweza kupata kitufe cha mapitio ya tiketi na vitu vingine vyenye uhusiano na shughuli za tiketi. Inafikiria kuwa sehemu ya kuanzia kazi za kila siku za wakala, kwa kawaida inatoa ufupisho wa haraka wa tiketi ambazo zinasubiri, zimepandishwa, mpya na zilizofunguliwa, kuachana nataarifa nyingine.

Moja ya sifa kubwa za Dashibodi ni kwamba inaweza kugeuzwa kabisa kukufaa. Hii inamaanisha unaweza kusanidi kila upande kadri utakavyo, kuonyesha au kuficha elementi. Pia inawezekana kuhamisha makazi ya hizi elemnti katika safuwima moja kwa kubofya na kukokota kichwa cha elementi, na kuzidondosha mahali pengine. Kila elementi ina jina "Kifaa", mfumo una baadhi ya vifaa vya kutumia nje ya boksi, lakini usanifu uliojikita kwenye moduli wa skrini ya dashibodi umeandaliwa kuunganisha vifaa vingine vya kawaida kwa urahisi.

Maudhui ya hii skrini imepangwa katika safuwima mbili kuu muhimu, kwenye safuwima ya kushoto unaweza kuona taarifa kuhusu tiketi zilizopangwa kwa hali zake kama: kikumbusho, iliyopandishwa, mpya, na wazi. Katika kila kifaa unaweza kuchuja matokeo kuona tiketi zote ambazo unaruhusiwa kufikia, tiketi ulizofunga, zile ambazo zipo kwenye foleni iliyofafanuliwa na wakala, pamoja na vichujio vingine. Pia kuna aina nyingine za vifaa katika hii safuwima na vimefafanuliwa chini.

Vifaa vya dashibodi vya safuwima ya kushoto.

Kwenye safuwima ya kulia kuna kifaa maalumu kinachokuruhusu kudhibiti vifaa unavyotaka kuonyesha au kuficha, Hiki ni kifaa cha Mipangilio. Bofya kwenye kichwa chake kupanua kifungu na kuona vifaa vyote vinavyopatikana, kama ilivyoonyeshwa kwenye Kielelezo. Kila jina la kifaa lina kisanduku tiki, Tumia hiki kisanduku tiki kufafanua muonekano wa vifaa katika dashibodi (vifaa visivyotikiwa havitaonyeshwa) baada ya kufafanua machaguo ya muonekano na kubofya "Hifadhi" kuhifadhi mabadiliko. Hiki kifungu kimefungwa sehemu moja katika skrini, hii inamaanisha huwezi kukikokota na kukiweka sehemu nyingine, au kukifunga.

Kielelezo: Mipangilio ya Dashibodi.

Vifaa vya dashibodi ya safuwima ya kulia.