Kutumia kisakinishi cha wavuti

Unaweza kutumia Kisakinishi cha Wavuti cha OTRS, baada ya kusakinisha programu ya OTRS, kuseti na kusanidi hifadhidata ya OTRS. Kisakinishi cha Wavuti ni ukurasa wa tovuti ambayo unaweza kuitembelea kwenye kivinjari chako. URL ya hicho kisakinishi cha wavuti ni http://localhost/otrs/installer.pl .

Pale kisakinishi cha wavuti kinapoanza, tafadhali fuata hatua zifuatazo kuseti mfumo wako:

1. Angalia taarifa kuhusu ofisi za OTRS na bofya kwenye inayofuata kuendelea (ona kielelezo chini).

Kielelezo: Skrini ya kukukaribisha.

2. Read the GNU GENERAL PUBLIC LICENSE (see Figure below) and accept it, by clicking the corresponding button at the bottom of the page.

Figure: GNU GENERAL PUBLIC LICENSE.

3. Chagua hifadhidata utakayotaka kutumia na OTRS. Kama ukichagua MySQL, PostgreSQL au Microsoft SQL kama Seva za hifadhidata, unaweza kuchagua kama utataka kisakinishi cha wavuti kikutengenezee hifadhidata yako au msimamizi wa hifadhidata wako ameshatengeneza hifadhidata tupu kwa ajili ya wewe kutumia. Baada ya hapo, bonyeza kitufe kuwndelea (ona kielelezo chini).

Kielelezo: Uchaguzi wa Hifadhidata.

4. Hii skrini inaweza kuwa tofauti kidogo kutegemeana na hifadhidata uliyochagua na kama ulitaka kisakinishi cha mtandao kutengeneza hifadhidata au kutumia iliyopo katika hatua iliyopita. Ingiza hati tambulishi za hifadhidata kwenye hii skrini.

Kielelezo: Hati tambulishi za hifadhidata.

5. Tengeneza mtumiaji mpya wa hifadhidata, chagua jina la hifadhidata na bofya kitufe cha kuendelea (ona Kielelezo chihi).

Warning

OTRS itatengeneza nywila imara kwa ajili yako. Inawezekana kuweka nywila yako mwenyewe kama ukitaka. Nywila itaandikwa kwenye faili la usanidi Kernel/Config.pm kwahiyo hakuna haja ya kukumbuka nywila hii.

Kielelezo: Mipangilio ya hifadhidata.

6. Hifadhidata itatengenezwa kama itahitajika, na kujazwa, kama ilivyoonyeshwa kwenye hii taswira. Bofya kitufe cha kuendelea kwenda kwenye skrini inayofuata.

Kielelezo: Uanzishaji hifadhidata kwa mafanikio.

7. Toa mipangilio yote ya mfumo na bofya kwenye kitufe cha kuendelea (ona Kielelezo chini).

Kielelezo: Mipangilio ya mfumo.

8. Kama ikihitajika, unaweza kutoa data zinazotakiwa kusanidi barua zinazoingia na zinazotoka , au kuruka hatua hii kwa kubonyeza kitufe cha kulia upande wa chini wa skrini (ona Kielelezo chini).

Kielelezo: Usanidi wa barua.

9. Hongera! Sasa usakinishaji wa OTRS umemalizika na unatakiwa kuweza kufanya kazi na mfumo (ona Kielelezo chini). Kuingia kwenye kilesura cha mtumiaji wa OTRS, tumia anwani http://localhost/otrs/index.pl kutoka kwenye kivinjari wavuti chako. Ingia kama msimamizi wa OTRS, kwa kutumia jina la mtumiaji 'root@localhost' na nywila iliyozalishwa. Baada ya hapo, unaweza kusanidi mfumo kufikia mahitaji yako.

Warning

Tafadhali andika nywila iliyozalishwa kwa ajili ya akaunti ya 'root@localhost'.

Kielelezo: Skrini ya mwisho ya kisakinishi cha wavuti.