Kutengeneza mandhari yako

Unaweza kutengeneza mandhari yako mwenyewe ili kutumia muonekano unaoupenda katika mazingira ya mbele ya tovuti ya OTRS. Kutengeneza mandhari yako, unatakiwa kugeuza matokeo ya violeza kwa mahitaji yako.

Taarifa zaidi kuhusu sintaksi na muundo wa violezo vinavyotoka zinapatikana katika Mwongozo wa Msanifu http://otrs.github.io/doc, hasa katika sura inayohusu violezo.

Kama mfano, fuata hatua zifuatazo kutengeneza mandhari mapya yanayoitwa "Kampuni":

  1. Tengeneza mpangilio orodha uitwao Kernel/Output/HTML/Company na nakili mafaili yote ambayo ungependa kubadilisha, kutoka Kernel/Output/HTML/Standard kwenda kwenye kabrasha jipya.

    Important

    Nakili mafaili yale tu utakayobadilisha. OTRS itapata kiotomatiki mafaili yasiyokuwepo kutoka kwenye maudhui ya Kawaida. Hii itafanya uboreshaji katika ngazi ya baadaye rahisi zaidi.

  2. Geuza kukufaa mafaili kwenye mpangilio orodha Kernel/Output/HTML/Company, na badilish amuonekano kwa mahitaji yako.

  3. Kamilisha mandhari mpya, ziongeze kwenye SysConfig kwenye Mazingira ya mbele::Mandhari.

Sasa mandhari mpya inatakiwa kuweza kutumika. Unaweza kuichagua kupitia kiungo chako cha kurasa ya mapendeleo binafsi.

Warning

Usibadilishe mafaili ya mandhari yaliyosafirishwa na OTRS, kwani haya mabadiliko yatapotea baada ya usasishaji. Tengeneza mandhari yako mwenyewe kwa kufuata hatua zilizoelezwa hapo juu.