The OTRS Scheduler is an independent system process that executes tasks in background. These kind of processes are know as daemons in Unix / Linux systems. It is independent but that doesn't mean that the Scheduler does everything alone, it is fully integrated into OTRS and can use any OTRS module as needed to complete each task.
Kwa sababu za akili ya kawaida mchakato wa Mratibu unahitaji kuanzishwa muda hadi muda. Hii inafanyika kiotomatiki na mchakato wa mratibu mwenyewe mara moja kwa siku, lakini inaweza kurekebishwa kama ikihitajika kwa kutumia SysConfig kwa kuhariri mpangilio "Mratibu::AnzishaupyaBaadaYaSekunde".
Mratibu wa OTRS ni mchakato otomatiki, binadamu anaingilia mchakato huu ili kuona hali yake mara kwa mara na kuanzisha au kusitisha mchakato.
Kama Mratibu akisitishwa kwa sababu yoyote, kazi zote zinazosubiri na mpya zilizosajiliwa wakati mratibu amesitishwa zitatekelezwa mara tu mratibu atakapoanzishwa tena (isipokuwa kama kazi zimesetiwa kutekelezwa hapo baadaye)
Mratibu haonekani katika Kiolesura cha Michoro cha Mtumiaji hadi kisitishe kufanya kazi.
Kuna taarifa za aina ambili tofauti kama mfumo ukitambua mratibu hafanyi kazi. Huu utambuzi unategemea ni mara ngapi usasishaji wa mchakato wa mratibu unafanyika. Kama tofauti kati ya muda wa sasa na muda wa mwisho wa usasishaji wa mchakato wa mwisho ni zaidi ya mara 2 ya usasishaji wa mchakato ujumbe wa onyo utaonyeshwa kwenye eneo la taarifa la OTRS . Kama ni zaidi ya mara 4 ya mchakato tahadhari itatolewa badala yake.
Muda wa kusasisha Mratibu wa mchakato unaweza kusanidiwa kupitia SysConfig kwenye mpangilio wa "Mratibu::PIDSasishaMuda".
Ukiona ujumbe wa onyo si lazima kuchukua hatua, lakini inashauriwa sana kukagua kama mratibu anafanya kazi. Kama ukiona tahadhari, basi kuna asilimia kubwa mratibu hafanyi kazi na inatakiwa kuanzishwa kwake.
Kwa kawaida taarifa ya Mratibu hafanyi kazi imewezeshwa, kama kuna huduma ya tovuti halali iliyosajiliwa katika hifadhidata, na inaonyeshwa kwa watumiaji wa kundi la "msimamizi" tu.
Kulemeza taarifa (haishauriwi) au kubadilisha au kuongeza makundi ya taarifa, tafadhali hariri mpangilio wa "Mazingira ya mbele::ModuliTaarifa###800-Mratibu-Kagua" katika SysConfig.
Kielelezo: Taarifa za mratibu.
Kwa ku bofya kiungo cha Mratibu hafanyi kazi (aidha onyo au tahadhari) kisanduku kidadisi kitafunguka kukuwezesha kuanza mchakato wa Mratibu tena. Mratibu anaweza kuanzishwa kwa kawaida au kwa lazima, kwa kubofya kwenye kisanduku tiki kinachohusika.
Kuanzisha Mratibu kwa lazima inahitajika endapo mchakato uliopita wa Mratibu ulisitishwa kwa hali isiyokuwa ya kawaida na Kitambulisho cha Mchakato bado kimesajiliwa kwenye hifadhidata.
Ili kuwa na udhibiti kamili wa Mratibu wa mchakato na kukagua hali yake halisi tafadhali tumia vifaa katika tungo amri kama ilivyoelezwa chini.
Kielelezo: Anzisha Mratibu.
Vifaa vya tungo amri ya Mratibu vinakuruhusu kudhibiti mchkato wa Mratibu (Kuanza / Kusitisha) au kuuliza hali yake. Pia kuna vifaa vya kusajili mchakato ili udhibitiwe na mfumo wa uendeshaji.
Included with OTRS there commandline interface (CLI) tools for the scheduler.
Mafaili ya init.d ni hati za kipekee ambazo huitwa na mfumo endeshi wakati wa kuanzisha na kuzima
OTRS inatoa hati za init.d kuanza / kusitisha mchakato wa Mratibu wa OTRS kiotomatiki kwa kutumia mfumo wa uendeshaji. Hati hizo zinapatikana chini ya OTRS_NYUMBANI/hati.
Hati za init.d zinahitaji kunakiliwa kwenda kwenye mahali sahihi kwa ajili ya mfumo endeshi wako. Zinahitaji kuwa na ruhusa sahihi na baadhi ya vishika nafasi vya ndani vinahitaji kusetiwa kufanya kazi vizuri. Kama ulitumia RPM za OTRS kuseti mfumo, hii inafanyika kiotomatiki.
Init.d Vishika nafasi vya Ndani vya Hati
OTRS_NYUMBANI - njia kwenda kwenye usanidi wa OTRS yako.
Mtumiaji - jina la mtumiaji wa mchakato wa apache.
Kundi - jina la kudni la mtumiaji wa apache.
Kwa sasa OTRS inatoa hati za init.d tu kwa majukwaa ya Linux.
Table 4.7. Orodha ya hati za init.d na mifumo endeshi inayotumika nayo
Hati ya Init | Mfumo endeshi unaokubalika |
---|---|
otrs-mratibu-linux | Red Hat, Fedora, CentOS, SUSE, openSUSE, Debian, Ubuntu |
otrs-scheduler-gentoo-init.d, otrs-scheduler-gentoo-conf.d | Gentoo |
Example 4.29. Mfano kuanzisha Mratibu wa OTRS kwenye linux
shell> /etc/init.d/otrs-scheduler-linux start
Vitendo vilivyopo.
anza Kuanza mchakato wa Mratibu wa OTRS.
sitisha kusitisha mchakato wa Mratibu wa OTRS.
anza upya kuanza upya mchakato wa Mratibu wa OTRS.
hali kuuliza hali ya mchakato wa Mratibu wa OTRS.
Mratibu anahitaji hifadhidata ipatikane kusajili kitambulisho chake cha Mchakato, kwasababu hii ni muhimu ku:
Tekeleza hati ya init.d ya Mratibu ili kuanza mchakato wa Mratibu baada ya mchakato wa hifadhidata kuamka na kuanza kazi.
Tekeleza hati ya init.d ya Mratibu ili kusitisha mchakato wa Mratibu baada ya mchakato wa hifadhidata kuzimwa.
Ukitaka Mratibu afanye kazi wakati wa uwashaji wa Mfumo, tafadhali soma waraka wa mfumo endeshi kujua sehemu sahihi ya kuweka hati za init.d, jinsi ya kufanya usanidi ziweze kuanza kiotomatiki na kuseti oda yao ya kazi.
Hii ni sehemu ya Mratibu inayobakia ikifanya kazi katika mazingira ya nyuma kukagua kazi za kutekeleza. Pia inatoa kazi za muhimu kudhibiti mchakato.
Unix / Linux zote zinatumia faili OTRS_HOME/bin/otrs.Scheduler.pl.
Machaguo Yaliyopo
-a kitendo.
Thamani ziwezekanazo
anza-kuanza mchakato wa Mratibu.
sitisha- kusitisha mchakato wa Mratibu.
hali- kuuliza hali ya mchakato wa Mratibu.
-f kulazimisha kuanza au kusitisha mchakato wa Mratibu.
Example 4.31. Mfano kulazimisha kusitisha Mratibu wa OTRS
shell> OTRS_HOME/bin/otrs.Scheduler.pl -a stop -f 1
Kusitisha Mratibu kwa lazima inatumika kuondoa kitambulisho cha mchakato kutoka kwenye hifadhidata wakati mratibu hafanyi kazi na mchakato bado umesajiliwa.
Kuanzisha Mratibu kwa lazima inatumika kuanza mchakato wa Mratibu kama mratibu hafanyi kazi na mchakato bado umesajiliwa.
Kuanzisha au kusitisha kwa lazima ni muhimu kama kuanza kwa mchakato kunahitajika kufanyika kabla ya muda wa kusasisha mchakato haujaisha. La sivyo ingizo lilokwisha muda wake kwenye hifadhidata linapuuzwa na uanzaji wa kawaida.