Hiki kitabu kimelenga kutumiwa na Wasimamizi wa OTRS. Pia ni ki rejeo kizuri kwa watumiaji wapya wa OTRS.
Sura zinazofwata zinaelezea usakinishaji, usanidi, na usimamizi wa progwamu ya OTRS. Theluthi moja ya kwanza ya nakala hii inaelezea kazi za muhimu za programu, wakati zinazobakia inafanya kazi kama marejeo ya seti nzima ya parameta zinazoweza kusanidiwa.
Hiki kitabu kinaendelea kuwa kazi iliyo kwenye mwendelezo, ikiwa lengo ni matoleo mapya. Tunahitaji maoni yenu ili kufanya hii nyaraka ya marejeo kuwa ya hali ya juu: ambayo inaweza kutumika, iko sahihi, na kamili. Tafadhali tuandikie kama unakuta kuna kitu hakipo kwenye hiki kitabu, kama vitu havijaelezewa kikamilifu, au kuna makosa ya kiuandishi na kisintaksia. Aina yoyote ya maoni yanathaminiwa na yanatakiwa kuwekwa kwenye mfumo wetu wa kufwatilia makosa katika http://bugs.otrs.org . Tunatanguliza shukrani kwa michango yenu.